-
Uwezo wa Iran wa kujihami angani umemfanya adui apoteze matumaini
Sep 01, 2019 06:55Brigedia Jenerali Alireza Sabahi Fard, Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya (SAW) cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akizingumza katika mkesha wa 'Siku ya Ulinzi wa Anga' ameashiria mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi wa anga na kusema: "Uwezo wa Iran wa kujihami angani umemfanya adui apoteze matumaini."
-
Iran yajibu vitisho vya Marekani: Tutauza mafuta kwa yeyote na kwa washitiri wote
Sep 01, 2019 03:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Marekani inatumia "uharamia na vitisho" kuizuia Iran isiuze mafuta yake, lakini Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuuza mafuta yake kwa yeyote na kwa wanunuzi wote.
-
Rouhani: Kama Ulaya hawatotekeleza ahadi zao, Iran itaanza awamu ya tatu ya kutotekeleza ahadi za JCPOA
Aug 31, 2019 22:47Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, usiku wa kuamkia leo amezungumza kwa simu na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na kusisitiza kuwa, kama nchi za Ulaya zitashindwa kutekeleza kivitendo ahadi zao, Tehran nayo itaanza kutekeleza awamu ya tatu ya kupunguza utekelezaji wa ahadi zake ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yaonyesha satalaiti, yakanusha madai ya Trump
Aug 31, 2019 11:51Iran imeonyesha hadharani satalaiti yake ya mawasiliano inayojulikana kama Nahid 1 na hivyo kukanusha madai ya Rais Donald Trump wa Marekani ambaye amedai kuwa satalaiti hiyo imeanguka wakati ilipokuwa inarushwa katika anga za mbali.
-
Sisitizo la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa EU juu ya kulinda makubaliano ya JCPOA na kuimarisha usalama wa Ghuba ya Uajemi
Aug 31, 2019 07:40Umoja wa Ulaya pamoja na Troika ya Ulaya zikiwa wanachama wa kundi la 4+1 mara kadhaa zimesisitiza kuwa kuna udharura wa kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na wakati huo huo kurejesha uthabiti na usalama katika Ghuba ya Uajemi kwa kuzingatia chokochoko za Marekani katika eneo hilo la maji lenye umuhimu wa kijio-stratejia.
-
Araqchi: Sharti la utekelezaji kamili wa JCPOA ni kudhaminiwa matakwa ya Iran
Aug 30, 2019 22:54Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesisitiza kuwa, ili Jamhuri ya Kiislamu irejee kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni lazima idhaminiwe matakwa yake kadhaa yakiwemo ya uuzaji mafuta pamoja na masuala ya kibenki yanayohusiana na uuzaji wa mafuta hayo.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Marekani ni kinara wa tawala za kigaidi duniani
Aug 30, 2019 07:29Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, Marekani ni kinara wa tawala za kigaidi kote duniani na kwamba, baada ya maafisa wa serikali ya Washington kukiri kwamba nchi hiyo ndiyo iliyoanzisha makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, ni aibu kubwa kwa Marekani kudai kuwa inapambana na ugaidi.
-
Zarif: Lazima Marekani isitishe ugaidi wa kiuchumi na irejee JCPOA, kabla ya mazungumzo
Aug 30, 2019 03:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema Marekani lazime irejee katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na isitishe ugaidi wake wa kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kabla ya kufanyika mazungumzo.
-
Iran na Syria, kuanzia vita dhidi ya ugaidi hadi kwenye ushirikiano wa kiuchumi
Aug 30, 2019 03:29Waziri wa Barabara na Ujenzi wa Iran amewasili katika mji mkuu wa Syria, Damascus kwa shabaha ya kufuatilia ushirikiano wa kiuchumi na kuchunguza njia za kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili.
-
Vikwazo vipya vya Marekani na woga wa Washington kuhusu nguvu za makombora za Iran
Aug 29, 2019 23:12Katika kipindi hiki cha utawala wa Donald Trump, Marekani imeliwekea taifa la Iran vikwazo vikubwa mno baada ya Washington kujitoa bila sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.