Araqchi: Sharti la utekelezaji kamili wa JCPOA ni kudhaminiwa matakwa ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55705-araqchi_sharti_la_utekelezaji_kamili_wa_jcpoa_ni_kudhaminiwa_matakwa_ya_iran
Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesisitiza kuwa, ili Jamhuri ya Kiislamu irejee kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni lazima idhaminiwe matakwa yake kadhaa yakiwemo ya uuzaji mafuta pamoja na masuala ya kibenki yanayohusiana na uuzaji wa mafuta hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 30, 2019 22:54 UTC
  • Araqchi: Sharti la utekelezaji kamili wa JCPOA ni kudhaminiwa matakwa ya Iran

Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesisitiza kuwa, ili Jamhuri ya Kiislamu irejee kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni lazima idhaminiwe matakwa yake kadhaa yakiwemo ya uuzaji mafuta pamoja na masuala ya kibenki yanayohusiana na uuzaji wa mafuta hayo.

Kuhusu mazungumzo na nchi za Ulaya na sisitizo lao la kulindwa JCPOA, Araqchi amesema, takwa la Iran liko wazi kabisa, hivyo kama nchi za Ulaya na nchi zingine wanachama wa JCPOA zinataka Iran irejee tena kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano hayo, inapasa zikidhi takwa la Jamhuri ya Kiislamu kuhusiana na uuzaji mafuta.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amebainisha kuwa, nchi za Ulaya ima ziyachukulie kibali mashirika yao kwa Marekani yanunue mafuta ya Iran, au kama haziwezi, serikali za nchi hizo ziiwezeshe Iran kuuza mafuta yake kwa kuipatia njia za itibari, itibari za usafirishaji mafuta hayo au ziidhaminie suala hilo kwa kutumia utaratibu mwingine wowote zitakaoona unafaa, kwa sababu bila kufanya hayo, haitawezekana Iran kurejea kwenye utekelezaji kamili wa JCPOA.

Araqchi aidha ameongezea kwa kusema: Siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya Marekani ni muqawama na kuhamasisha kwa kiwango cha juu kabisa utumiaji wa suhula zake.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ulaya, walisisitiza katika taarifa waliyotoa baada ya kikao walichofanya hapo jana mjini Helsinki, Finland juu ya ulazima wa kulindwa makubaliano ya nyuklia na Iran ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).../