-
Saudia: Israel inahatarisha usalama na utulivu wa eneo zima
Mar 20, 2025 03:12Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatishia usalama na utulivu wa eneo hili zima na kwamba jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama zina wajibu wa kutekeleza majukumu yao ipaswavyo na kusimama kidete kukabiliana na hujuma za Israel huko Palestina na Syria.
-
Netanyahu: Mashambulio yalioua watoto 174 Gaza ni mwanzo tu
Mar 19, 2025 23:40Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kushadidi mashambulio mabaya dhidi ya Gaza, akionya kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya anga, ambayo yaliua watoto wasiopungua 174 katika ukanda huo, ni mwanzo tu wa uchokozi mkubwa zaidi dhidi ya Wapalestina.
-
Dunia yakasirishwa na hatua ya Israel kuendeleza vita dhidi ya Gaza
Mar 19, 2025 08:35Jamii ya kimataifa imebainisha hasira yake baada ya utawala katili wa Israel kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
-
Al Houthi: Israel inapanga kushambulia nchi zingine ikiwa itaangamiza Palestina
Mar 19, 2025 08:28Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuwa utawala ghasibu wa Israel utaanza kushambulia nchi nyingine ikiwa utafanikiwa kuangamiza juhudi za ukombozi za Palestina dhidi ya ukaliaji na uchokozi wake, huku akipendekeza hatua za kijeshi na nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya utawala huo.
-
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza
Mar 19, 2025 04:11Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.
-
Maafisa 5 waandamizi wa HAMAS wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel Ghaza
Mar 19, 2025 00:44Maafisa watano waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
'Waislamu wachukue msimamo wa maana dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni'
Mar 19, 2025 00:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya An-Nujabaa imelaani mashambulizi ya kinyama yaliyoanzishwa tena na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuwataka Waarabu na Waislamu duniani kote wachukue misimamo thabiti dhidi ya hujuma hizo.
-
Baada ya jinai mpya za Ghaza, sasa milango ya mashimo ya kujifichia Wazayuni imefunguliwa Tel Aviv
Mar 18, 2025 08:00Leo Jumanne, viongozi ya Israel wamelazimika kufunga milango mashimo na mahandaki wanayojifichia Wazayuni baada ya utawala wa Kizayuni kufanya jinai mpya Ghaza. Wazayuni wameingiwa na hofu kubwa ya makundi ya Muqawama kulipiza kisasi cha jinai za usiku wa kuamkia leo za Israel huko Ghaza.
-
UN yataka kila mwenye ushawishi azuie mashambulizi ya Israel huko Ghaza
Mar 18, 2025 08:00Tom Fletcher, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu ameonesha hisia zake kuhusu taarifa za kutisha za mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Ghaza, akisema kuwa, kila mwenye ushawishi ana wajibu wa kufanya kadiri awezavyo kukomesha jambo hilo.
-
Israel yashambulia upya Gaza, yaua mamia ya Watoto na wanawake
Mar 18, 2025 04:14Jeshi la utawal katili wa Israel limeua Wapalestina wasiopungua 350, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, katika maeneo yote ya Ukanda wa Gaza wakati wa ukiukwaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Tel Aviv na vikosi vya Muqawama vya Palestina vilivyoko Gaza.