-
Katibu Mkuu wa UN: Ghaza ni uwanja wa mauaji, kuwahamisha Wapalestina hakukubaliki
Apr 09, 2025 03:07Katika tamko kali zaidi ambalo amewahi kutoa hadi sasa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa indhari kuhusu hali ya janga la kibinadamu inayozidi kuwa mbaya katika Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas yafananisha vitendo vya Israel Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda
Apr 08, 2025 23:35Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imefananisha vitendo vya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda, huku ikisifu hatua ya Umoja wa Afrika ya kumfukuza balozi wa utawala wa Israel kutoka mkutano maalumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
-
Israel yampiga marufuku mkurugenzi wa Msikiti wa Ibrahimi kwa siku 15
Apr 08, 2025 23:02Utawala haramu wa Israel umempiga marufuku mkurugenzi wa Msikiti wa Ibrahimi ulioko katika mji wa al-Khalil, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kuingia katika eneo hilo takatifu la Kiislamu kwa zaidi ya wiki mbili, huku utawala huo ukiendeleza mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.
-
Ndege za kivita za Marekani zashambulia Yemen karibu mara 30 katika muda wa chini ya siku moja
Apr 08, 2025 06:47Marekani imefanya karibu mashambulizi 30 ya anga katika majimbo kadhaa kote nchini Yemen katika muda wa chini ya siku moja, na kushadidisha uchokozi wake dhidi ya taifa hilo, katika kile ambacho wataalamu wamekitaja kuwa ni harakati za kujishinda yenyewe za kusitisha bila mafanikio operesheni za Sana'a zinazotekelezwa dhidi ya Israel na waungaji mkono wake kwa ajilii ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Mashirika sita ya UN: Vita vya Ghaza ni ishara ya kutojaliwa hata chembe maisha ya binadamu
Apr 08, 2025 06:21Wakuu wa mashirika sita ya Umoja wa Mataifa wametoa indhari kali kuhusu hali ya Ukanda wa Ghaza na kutaka usitishaji vita utekelezwe tena na kwa haraka sana, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya katika eneo hilo linaloendelea kuandamwa na mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Msemaji wa Taliban: Askari wa Marekani hawawezi kuruhusiwa kuwepo ndani ya ardhi ya Afghanistan
Apr 08, 2025 06:11Msemaji wa serikali ya muda ya Afghanistan amesisitiza kuwa haiwezekani askari wa Marekani waruhusiwe kwenda na kuwepo ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Waisraeli waandamana kupinga kuanza tena vita vya Gaza
Apr 08, 2025 03:11Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya Tel Aviv kushiriki katika maandamano mapya ya kupinga serikali ya utawala haramu wa Israel, wakati ambapo Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu alipokutana na Rais wa Marekani, Donald Trump mjini Washington.
-
Watoto laki 6 wa Kipalestina Gaza katika hatari ya kupata ulemavu
Apr 07, 2025 08:06Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imesema hatua ya Israel ya kuzuia kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza wa polio inawaweka malaki ya watoto wa Kipalestina katika hatari ya kupata ulemavu wa kudumu.
-
Hamas yapongeza wafanyakazi Microsoft kwa kufichua ushiriki wa kampuni hiyo katika mauaji ya kimbari Gaza
Apr 06, 2025 23:16Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeelezea kufurahishwa na misimamo ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Microsoft wakati wa sherehe ya miaka 50 ya kampuni hiyo ya teknolojia wakipinga ushiriki wa Microsoft katika vita vya mauaji ya halaiki vya jeshi la Israeli katika Ukanda wa Gaza.
-
Kusimama imara muqawama wa Yemen kumeleta mabadiliko yapi Asia Magharibi?
Apr 06, 2025 23:14Vikosi vya ulinzi vya Yemen vinaendelea kutekeleza oparesheni katika Bahari Nyekundu na katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel); na hatua za muqawama wa Yemen zimekuwa na taathira kwa matukio ya kanda hiyo ya Magharibi mwa Asia.