-
UN: Asilimia 100 ya Gaza ni mali ya Wapalestina, yataka Israel ikomeshe uvamizi haramu
May 30, 2026 10:29Umoja wa Mataifa umekosoa vikali mipango ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ya kupanua udhibiti juu ya Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kuwa eneo lote ni haki ya watu wa Palestina.
-
Kwa nini utawala wa Kizayuni unasisitiza kuendeleza vita huko Lebanon?
May 30, 2026 07:00Moja ya vikwazo muhimu katika mazungumzo ya Iran na Marekani ni sisitizo la utawala wa Kizayuni wa Israel la kuondolewa medani ya vita vya Lebanon kwenye mazungumzo hayo na kuendeleza vita dhidi ya harakati ya Hizbullah. Hii ni katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa moja ya masharti muhimu ya kufikiwa mapatano na Marekani ni kusimamishwa kikamilifu vita katika ngome zote za mhimili wa muqawama na hasa nchini Lebanon.
-
Hizbullah: Hakuna njia nyingine isipokuwa mapambano dhidi ya Israel
May 30, 2026 03:27Mbunge mwandamizi wa Lebanon amesema kuwa harakati ya Hizbullah itaendeleza operesheni zake za kijeshi dhidi ya vikosi vya utawala dhalimu wa Israel.
-
IRIB yalaani mauaji ya Israel dhidi ya mwandishi habari wa al-Alam kusini mwa Lebanon
May 29, 2026 12:39Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), Peyman Jebelli, na Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha IRIB wamelaani vikali mauaji ya Hesam Zidan, mwandishi wa habari wa zamani wa chaneli ya televisheni ya al-Alam ya Iran nchini Syria, ambaye ameuawa katika shambulio la Israel kusini mwa Lebanon.
-
UN yaanika uhalifu wa kutisha wa Israel... Ripoti ya Guterres kuhusu unyanyasaji wa kingono imefichua nini?
May 29, 2026 12:38Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Alkhamisi ya jana aliwasilisha ripoti yake ya kila mwaka kwa wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro, ambayo inarekodi ukiukwaji mkubwa na wa kutisha wa sheria uliofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.
-
Washington Post: Israel imetengwa duniani kutokana na vita vya mara kwa mara vya Netanyahu
May 29, 2026 02:57Gazeti la Washington Post limeandika kuwa: Vita vya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, Lebanon, Syria, Iran na Yemen vimeiweka Israel katika njia ya mmomonyoko wa kijeshi, kushindwa kimkakati na kutengwa kimataifa.
-
Al-Houthi: Umma wa Kiislamu unapaswa kujifunza kutokana na mapambano ya Iran dhidi ya Marekani na Israel
May 28, 2026 04:48Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa: Msimamo imara wa Iran unapaswa kuwa kichocheo cha kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
-
Ma'ariv: Maafisa 50 wa utawala unaotaka kujitenga Somaliland wamepewa nafunzo Israel
May 28, 2026 04:43Gazeti la Kiebrania la Ma'ariv limefichua kashfa mpya kuhusu uhusiano wa siri kati ya Tel Aviv na eneo linalotaka kujitenga huko kaskazini mwa Somalia, likiandika kwamba askari 50 wa "Somaliland" wamerejea Afrika baada ya kukamilisha kozi za mafunzo katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
Kwa nini Trump anataka Pakistan iwe na uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel?
May 27, 2026 13:29Chanzo kimoja cha habari cha Pakistan kimeripoti kuhusu upinzani wa wazi wa Islamabad dhidi ya ombi la Rais Donald Trump wa Marekani la kuitaka nchi hiyo ijiunge na mchakato wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, na kuongeza kuwa Islamabad inaiona hatua ya Washington kuwa jaribio la kutumia vibaya diplomasia ya "kusimamisha vita na Iran" ili kutoa mashinikizo katika kesi zisizohusiana.
-
Hizbullah yatekeleza operesheni 32 dhidi ya majeshi ghasibu ya Israel kusini mwa Lebanon
May 27, 2026 10:51Harakati ya Mapambano ya Kiislamu nchini Lebanon, Hizbullah, imetangaza kutekeleza mfululizo wa operesheni 32 za kijeshi dhidi ya majeshi vamizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yanayofanya chokochoko kusini mwa nchi hiyo.