-
Wapalestina wa Gaza katika jinamizi badala ya sherehe wakati wa Eid el-Adha
May 27, 2026 10:43Ikiwa leo ni sikukuu ya Eid El-Adha, Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel hawana cha kusherehekea bali wanakumbwa na jinamizi na masaibu yaliyosababishwa na utawala huo ghasibu.
-
Pakistan yakataa wito wa Marekani wa kuanzisha uhusiano na 'Israel'
May 27, 2026 03:12Pakistan imekataa wito wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wa kuitaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel. Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, Khawaja Asif, amesema pendekezo hilo kuwa “halikubaliki” na linakwenda kinyume na misingi ya taifa hilo.
-
Nabih Berri: Kwa pamoja tutaikomboa na kuijenga upya Lebanon
May 25, 2026 14:22Katika siku ya kumbukumbu ya kukombolewa Lebanon kutoka kwenye makucha ya utawala ghasibu wa Israel, Nabih Berri, Spika wa Bunge la nchi hiyo amesema kuwa, adui Mzayuni hatasita hata kidogo kulipiza kisasi dhidi ya Lebanon na kuongeza kwamba kwa pamoja watu wa nchi hiyo wana uwezo wa kuikomboa na kuijenga upya.
-
Malaysia: Tutaipeleka Israel ICJ kwa kuteka nyara na kuwatesa wanaharakati wa Freedom Flotilla
May 25, 2026 12:21Serikali ya Malaysia iko tayari kuipeleka Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa kosa la kuteka nyara na kuwatesa wanaharakati wa msafara meli za misaada ya kibinadamu wa Global Sumud Flotilla, uliokuwa njiani kuelekea Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Muqawama wa Palestina utaikomboa al-Qud: Jenerali Qa’ani
May 25, 2026 12:19Kamanda mkuu wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Muqawama wa Palestina utafungua njia ya ukombozi wa al-Quds, ukiashiria ushindi wa harakati za Muqawama nchini Iran na Lebanon.
-
Afisa wa zamani wa Kizayuni: Hatimaye tutatoroka Lebanon kwa madhila
May 25, 2026 12:02Mkuu wa zamani wa Kamati ya Usalama na Mahusiano ya Kigeni katika Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kwamba utawala huo hatimaye utatoroka Lebanon kwa madhila na kushindwa.
-
Makumi wauawa katika shambulio la bomu lililolenga kituo cha treni Pakistani
May 24, 2026 13:11Shambulio la kigaidi katika kituo cha treni katika mji mkuu wa jimbo la Balochistan nchini Pakistani limesababisha vifo vya watu 24 na kujeruhiwa wengine wengi.
-
Israel yawazuia tena Wapalestina wa Gaza kutekeleza ibada ya Hija
May 24, 2026 12:43Watetezi wa haki za binadamu na maafisa wa Palestina wamelaani hatua wanayoieleza kuwa ni kukiuka kwa mfumo uhuru wa ibada, baada ya utawala haramu wa Israel kwa mara nyingine kuzuia maelfu ya Wapalestina wa Gaza kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hija ya kila mwaka.
-
MEE: Misri iliishinikiza Al-Azhar 'kuunga mkono UAE' katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran
May 23, 2026 02:43Ripoti zinasema kwamba Ofisi ya Rais wa Misri iliishinikiza taasisi ya Al-Azhar, ambayo ni mamlaka ya juu zaidi ya Waislamu wa madhehebu ya Suni, kuunga mkono hadharani Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na mataifa mengine ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Picha za satalaiti zaonyesha uharibifu mkubwa kwenye kambi za kijeshi za Israel kutokana na mashambulizi ya Iran
May 22, 2026 14:53Picha mpya za satalaiti zilizochambuliwa zimefichua uharibifu na hasara kubwa iliyotokea katika vituo vingi vya kijeshi vya Israel kufuatia mashambulizi na operesheni za kujihami za Iran na harakati ya Lebanon Hizbullah na hivyo kuzusha maswali kuhusu ukubwa wa uharibifu ambao Tel Aviv inauficha mbele ya umma.