Israel yawazuia tena Wapalestina wa Gaza kutekeleza ibada ya Hija
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i138602-israel_yawazuia_tena_wapalestina_wa_gaza_kutekeleza_ibada_ya_hija
Watetezi wa haki za binadamu na maafisa wa Palestina wamelaani hatua wanayoieleza kuwa ni kukiuka kwa mfumo uhuru wa ibada, baada ya utawala haramu wa Israel kwa mara nyingine kuzuia maelfu ya Wapalestina wa Gaza kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hija ya kila mwaka.
(last modified 2026-05-24T12:52:51+00:00 )
May 24, 2026 12:43 UTC
  • Israel yawazuia tena Wapalestina wa Gaza kutekeleza ibada ya Hija

Watetezi wa haki za binadamu na maafisa wa Palestina wamelaani hatua wanayoieleza kuwa ni kukiuka kwa mfumo uhuru wa ibada, baada ya utawala haramu wa Israel kwa mara nyingine kuzuia maelfu ya Wapalestina wa Gaza kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hija ya kila mwaka.

Maelfu ya Wapalestina wa Gaza wameshindwa tena kutekeleza ibada ya Hija huku Israel ikiendelea kuweka vikwazo vya usafiri kupitia mipaka ya Gaza.

Wakati Waislamu kutoka pembe zote za dunia wakifika Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ambayo ni miongoni mwa nguzo za Uislamu, wengi wa Wapalestina wa Gaza wanasalia wakiwa wamekwama kutokana na vita, mzingiro na ukimbizi.

Kufungwa kwa vituo vya mpakani na janga la kibinadamu lililotokana na vita kumewanyima maelfu ya Wapalestina fursa ya kutekeleza moja ya nguzo muhimu zaidi za dini ya Uislamu.

Rami Abu Staitah, Mkurugenzi Mkuu wa Hija na Umra katika Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kidini ya Gaza, amesema kuwa Palestina hupokea mgao wa mahujaji 6,600 kwa mujibu wa makubaliano na Saudi Arabia, na Gaza ikipata takribani asilimia 38 ya nafasi hizo.

Kulingana na Abu Staitah, Wapalestina 2,473 kutoka Gaza walikuwa wamepitia mfumo wa bahati nasibu wa Hija tangu 2013 na walikuwa wakisubiri zamu yao.

Amesema kuwa 71 walifariki kabla ya kufikia safari ya Hija, wengine katika mashambulizi, wengine kwa sababu za kawaida, na 2,402 wanasalia bila uwezo wa kusafiri.

Abu Staitah amebaini kuwa kuendelea kwa hali hii ni “pigo kubwa” kwa Waislamu wa Gaza. Wananchi wengi wanaendelea kuwasiliana na Wizara ya Awqaf kuhakikisha majina yao bado yanasalia kwenye orodha, wakitumaini kuwa siku moja wasafiri wataweza kuruhusiwa.

Kabla ya vita, mahujaji wa Gaza walikuwa wakivuka kupitia mpakani wa Rafah kuelekea Misri, kisha Cairo, na baadaye Saudi Arabia.

Mchakato huo ulihusisha uratibu kati ya viongozi wa kidini wa Kipalestina pamoja na maafisa wa Misri na Saudi Arabia.

Hata hivyo, utawala wa Israel uliteka na kufunga upande wa Kipalestina wa mpakani wa Rafah mnamo Mei 2024, na kuikata Gaza kutoka njia yake ya mwisho ya moja kwa moja kuelekea ulimwengu wa nje.

Kwa Wapalestina wengi, kushindwa kutekeleza Hija hakumaanishi tu kikwazo cha kiutendaji, bali pia ni sura nyingine ya maumivu ya muda mrefu na hali ya kutokuwa na uhakika chini ya mazingira ya vita na mzingiro unaoongezeka.