-
Kiongozi mkuu wa kidini wa Bahrain alaani mataifa ya Kiarabu kwa kutumikia ajenda za Marekani na Israel
Aug 03, 2026 10:08Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain, amezilaani nchi za Kiarabu na Kiislamu za kanda ya Magharibi mwa Asia kwa kuchangia katika njama za Marekani na Israel za kuimarisha migawanyiko katika eneo hilo.
-
Malengo ya Julani katika kuanzisha uadui dhidi ya kundi la Hashd al-Shaabi la Iraq
Aug 03, 2026 08:39Abu Mohammad al-Julani, mtawala wa serikali ya mpito ya Syria, amedai katika matamshi tatanishi kuwa ana wasiwasi kuhusu uwepo wa makundi ya wanamgambo wa Iraq na vikosi vya Hashd al-Shaabi katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
-
Maandamano makubwa ya kupinga sera zilizofeli za Benjamin Netanyahu
Aug 03, 2026 02:40Wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel wamefanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali wakipinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo wamezitaja kuwa zimeshindwa.
-
Katika mwezi wa Julai pekee Israel imeua Wapalestina zaidi ya 150 Ghaza
Aug 02, 2026 13:10Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza kuwa, katika mwezi Julai pekee, Wapalestina 152 waliuawa shahidi katika eneo hilo lililowekewa mzingiro, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo vya kila mwezi kuwahi kurekodiwa tangu ulipoanza mwaka huu.
-
Vita vya kinyama vya Israel Ghaza: Miili 40 ya watoto, 38 ya wanawake miongoni mwa iliyotolewa kwenye kifusi
Aug 02, 2026 12:57Shirika la Ulinzi wa Raia la Ghaza limesema, wafanyakazi wake walipata miili na mabaki ya watu 112 kutoka chini ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa na mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel katika kitongoji cha Sabra cha Jiji la Ghaza.
-
Changamoto mpya kwa Wasaudia kufuatia mzingiro wa majini wa Yemen
Aug 02, 2026 11:03Mzingiro wa majini wa Yemen dhidi ya Saudi Arabia, pamoja na kufungwa kwa Lango-Bahari la Bab al-Mandab kwa meli za mafuta za Saudia, vimetoa changamoto mpya kwa Wasaudia.
-
Mazuwari zaidi ya milioni nne wameingia Iraq tangu Muharram hadi sasa
Aug 02, 2026 03:27Mkuu wa Idara ya habari ya masuala ya usalama wa Iraq ametangaza kuwa wafanyaziara zaidi ya milioni nne wa kigeni wamewasili nchini humo tangu mwanzo wa mwezi wa Muharram, na kwamba zoezi la upokeaji mazuwari wanaokwenda kushiriki kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS lingali unaendelea.
-
Shambulio la Israel dhidi ya maghala ya dawa Ghaza latajwa kuwa ni 'jinai ovu sana'
Aug 02, 2026 02:42Wizara ya Afya ya Ghaza imelaani kile ilichokiita "jinai ovu sana" iliyofanywa na vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel huko Deir el-Balah, ikisema shambulio hilo la Ijumaa asubuhi lililenga "maghala ya dawa" ya Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa, na kuyabomoa kikamilifu mawili kati ya maghala hayo.
-
Meja Jenerali Abdullahi: Sasa, majeneza ni sehemu ya vifaa vya wanajeshi wa Marekani, Asia Magharibi
Aug 01, 2026 06:35Mkuu wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Khatamul-Anbiya (SAW) ameandika ujumbe katika mitandao ya kiijamii akisema: Majeneza ya Wamarekani sasa ni sehemu ya vifaa vyao katika eneo la Asia Magharibi.
-
Jeshi la Yemen lalazimisha meli 8 za mafuta za Saudia kubadili njia
Aug 01, 2026 06:33Msemaji wa Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen ametangaza katika taarifa kwamba, katika juhudi za kuimarisha mlingano wa “kuzingirwa kwa kuzingirwa”, na kufuatia kuongezeka kwa vikwazo vya baharini dhidi ya meli za mafuta za Saudi Arabia, meli nane za mafuta za Saudi Arabia zimelazimika kubadili njia na kuelekea Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope).