Muqawama wa Palestina utaikomboa al-Qud: Jenerali Qa’ani
-
Brigedia Jenerali Esmail Qa’ani
Kamanda mkuu wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Muqawama wa Palestina utafungua njia ya ukombozi wa al-Quds, ukiashiria ushindi wa harakati za Muqawama nchini Iran na Lebanon.
Brigedia Jenerali Esmail Qa’ani ameashiria ukombozi wa Khorramshahr, kusini magharibi mwa Iran, Mei 24, 1982 wakati wa vita vya Iran-Iraq, ambavyo amesema viliweka msingi wa "hamasa adhimu" ya Mei 25, 2000, wakati Hizbullah ilipofanikiwa kuufukuza utawala wa Israel kutoka kusini mwa Lebanon.
"Wakati wa kukimbia huko, jeshi la Israel liliacha redio zao zikiwa bado zinawaka, na zana zao zote ziliachwa nyuma kwenye mitaro," amesema Qa'ani.
Brigedia Jenerali Qa’ani amehitimisha kwa kusema kwamba, Muqawama wa "Palestina pendwa na Lebanon shujaa" pia utapelekea kukombolewa Al-Quds.
Jana, Mei 24, Iran iliadhimisha kumbukumbu ya ukombozi wa Khorramshahr hapo mwaka wa 1982 baada ya siku 578 za uvamizi wa Iraq wakati wa Vita vya Kulazimishwa vilivyodumu miaka minane.
Ushindi huo mkubwa ulipatikana katika Operesheni Bait al-Moqaddas, baada ya siku 578 za kukaliwa na Jeshi la Ba’ath la Iraq.
Nchini Lebanon, utawala wa Israel uliondoa vikosi vyake katika maeneo ya kusini Mei 25, 2000, baada ya miaka 22 ya uvamizi, baada ya kushindwa kwa madhila kwa vipigo vya harakati za ya Hizbullah ya Israel.