-
Jeshi la Israel lawaua kwa kuwapiga risasi watoto wa miaka 12 na 13 Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Feb 22, 2025 02:34Watoto wawili wa Kipalestina wenye umri wa miaka 12 na 13 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa mfululizo wa mashambulizi mengi yaliyofanywa na jeshi hilo usiku kucha wa kuamkia leo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yakijumuisha maeneo ya Tulkarem, Jenin na Nablus.
-
Israel yampiga marufuku msomi maarufu wa Kiislamu kuingia Msikiti wa Al-Aqsa
Feb 21, 2025 23:41Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimemkamata na kumpiga marufuku Sheikh Najeh Bakirat, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu Palestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa ulioko jijini Al Quds (Jerusalem).
-
UN: Inahitajika zaidi ya nusu karne kuufufua uchumi wa Syria urejee kwenye hali ya kabla ya vita
Feb 21, 2025 23:32Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Syria inahitaji muda wa zaidi ya nusu karne ili kurejea kwenye hali yake ya uchumi ya kabla ya vita angamizi vya ndani ya nchi hiyo.
-
Mateka wa Kizayuni: Kwa muda wote walipotushikilia, Al-Qassam waliamiliana nasi kwa wema
Feb 21, 2025 07:27Gazeti moja la Kizayuni limemnukuu mateka mmoja Muisrael akisema kuwa Wanamuqawama wa Brigedi za al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS waliamiliana kwa wema na mateka hao wa Kizayuni kwa muda wote walipokuwa wakiwashikilia huko Ukanda wa Ghaza.
-
Netanyahu adai mabaki ya mwili yaliyorejeshwa si ya Shiri Bibas, HAMAS yamjibu
Feb 21, 2025 07:24Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amedai kuwa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekiuka masharti ya makubaliano ya kubadilishana mateka kwa sababu imekabidhi mwili wa mwanamke asiyejulikana kutoka Ghaza badala ya ule wa mateka wa Kizayuni Shiri Bibas.
-
Askofu Mkuu wa Quds: Palestina, kamwe haitomsahau Nasrullah
Feb 21, 2025 03:21Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki katika mji mtukufu wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu, Atallah Hanna, amemuenzi na kumsifu aliyekuwa Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasralluh, akisisitiza kuwa watu wa Palestina daima wataendelea kuwa waaminifu kwake kwa namna alivyojitolea muhanga.
-
Ripoti ya Human Rights Watch yafichua jinai ya kutisha ya Israel
Feb 20, 2025 22:54Shirika la haki za binadamu la Humar Rights Watch limetoa ripoti mpya inayoonesha ukatili na jinai kubwa ya kuchupa mipaka iliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas: Israel iliua mateka wake kwa kulipua vituo walikokuwa wamezuiliwa
Feb 20, 2025 07:59Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema leo Alkhamisi kwamba, tawi lake la kiijeshi Izuddin al Qassam na muqawama kwa ujumla vina wamefanya kila liwezekanalo kulinda heshima ya maiti wakati wa shughuli ya kukabidhi miili ya matekka hao, ilhali utawala vamizi wa Isarel haukuheshimu uhai yao walipokuwa hai.
-
Oxfam: Tunaanza kuelewa kina cha uharibifu uliofanyika Gaza
Feb 20, 2025 07:55Shirika la Oxfam la Uingereza limetangaza kuwa utawala wa Israel umeharibu zaidi ya asilimia 80 ya mitandao ya maji na maji taka ya Gaza na kusababisha hali mbaya ya kiafya.
-
Euro-Med: Israel inatumia drone kuwatia hofu watu wa Gaza, inawatisha kwa 'Nakba ya 2, ya 3'
Feb 20, 2025 07:50Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor limeonya kuwa utawala wa Kizayunii wa Israel unatumia ndege zisizo na rubani kama silaha ya kisaikolojia kuwatia hofu na wahka Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na hivyo kuzidisha mashinikizo kwa wakazi wa eneo hilo ili wakubali mpango wa Marekani na Israel unaowalazimisha kuhama makazi yao.