-
Wanajeshi 30 wa Kizayuni waangamizwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Nov 18, 2024 23:14Kwa akali wanajeshi 30 wa utawala haramu wa Israel wameangamizwa na wanamuqawama kaskazini mwa Ukanda wa Gaza katika majuma ya hivi karibuni.
-
Yemen yatoa taarifa kuhusu mashambulizi iliyofanya dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni
Nov 18, 2024 03:45Jeshi la Yemen limetoa taarifa kuhusu mashambulizi liliyofanya dhidi ya baadhi ya maeneo nyeti na muhimu sana ya kijeshi ya adui Mzayuni katika maeneo ya Jaffa na Ashkelon huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopachikwa jina bandia la Israel.
-
Hamas yalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Beit Lahiya
Nov 17, 2024 23:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imelaani mashambulizi makali yaliyofanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya jengo la makazi ya raia na kuua makumi ya watu katika Ukanda wa Gaza. Taarifa iliyotolewa na Hamas imesisitiza kwamba vitendo hivyo vya kichokozi havitavunja irada na azma thabiti ya watu wa Palestina.
-
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani atoa mwito wa uchunguzi wa mauaji ya kimbari Gaza
Nov 17, 2024 23:05Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa mwito wa kufanyika uchunguzi wa jamii ya kimataifa kuhusu "mauaji ya halaiki" ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Bin Salman aakhirisha kushiriki mkutano wa G20 kwa matatizo ya kiafya
Nov 17, 2024 23:05Shirika la Habari la Bloomberg limetangaza kuwa, Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman ameghairi safari yake iliyokuwa imepangwa ya kushiriki mkutano wa kilele wa viongozi wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayostawi kiuchumi la G20, unaoanza leo (Jumatatu) huko Rio de Janeiro, Brazil.
-
Human Rights Watch yakiri kuhusika utawala wa Kizayuni wa Israel na jinai za kivita
Nov 17, 2024 23:04Katika ripoti yake ya hivi karibuni zaidi, shirika la kuteteta haki za binadamu la Human Rights Watch kwa mara nyingine tena limetangaza kuwa utawala haramu wa Israel umefanya jinai za kivita dhidi ya binadamu na mauaji ya kikabila huko Gaza, kuharibu vyanzo vya maisha na kuwafanya kuwa wakimbizi mara kadhaa asilimia 90 ya wakaazi wa Gaza.
-
Msemaji wa Hizbullah auawa shahidi katika shambulio la kinyama la Israel
Nov 17, 2024 11:19Mohammad Afif, afisa wa habari wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameuawa shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni huko Ras al-Naba, Beirut mji mkuu wa Lebanon.
-
Israel yafanya mauaji mengine ya halaiki Ghaza, yawaua shahidi Wapalestina wasiopungua 96
Nov 17, 2024 09:34Wapalestina wasiopungua 96 wameuawa shahidi na wengine 60 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kinyama ya anga yaliyofanywa leo na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kaskazini na katikati mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Katika muda wa siku moja, jeshi la Kizayuni lafanya mashambulio 145 nchini Lebanon
Nov 17, 2024 09:11Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limefanya mashambulizi 145 nchini Lebanon katika muda wa saa 24 zilizopita huku likishaidisha hujuma zake za kinyama dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu kinyume na wito wa kimataifa wa kuutaka utawala huo haramu usimamishe mashine yake ya mauaji katika eneo hili la Asia Magharibi.
-
Makazi ya Netanyahu yarushiwa moto, inadhaniwa ni hujuma ya wapinzani wake wa ndani
Nov 17, 2024 04:19Mapema usiku wa kuamkia leo, moto umerushwa katika makazi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, huko Caesarea, tukio lililoelezwa kuwa ni "kuongezeka kwa hatari."