-
UN yalaaani vikali kitendo kisicho cha kimaadili cha mwakilishi wa Israel
Jun 08, 2024 23:48Stéphane Dujarric, Msemaji Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali hatua isiyo ya kimaadili ya mwakilishi wa utawala wa Kizayuni baada ya umoja huo kuamua kuiweka Israel katika orodha ya madola yanayofanya uhalifu wa kivita na kuua watoto wadogo.
-
"Netanyahu ni kichaa; kichaa chake hakitibiki, yeye na mkewe na mwanawe"
Jun 08, 2024 23:47Baada ya waziri mkuu wa Israel, kutoa amri ya kuuliwa kwa umati na kujeruhiwa Wapalestina 610 kwa mkupuo mmoja, watu wengi wamesisitiza kuwa Benjamin Netanyahu ana maradhi ya kichaa kibaya cha kunusa damu za watu wasio na hatia.
-
Jeshi la Kizayuni laua shahidi Wapalestina 210 katika 'shambulio la kikatili lisilowahi kushuhudiwa' kwenye kambi ya Nuseirat
Jun 08, 2024 07:50Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imesema, askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya "shambulio la kikatili ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat" na kuua kwa umati Wapalestina 210 hadi hivi sasa na makumi ya watu kujeruhiwa mitaani.
-
Netanyahu akasirika UN kuliweka jeshi 'lenye maadili zaidi' la Israel kwenye orodha ya wauaji wa watoto
Jun 08, 2024 07:18Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekasirishwa sana na hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuliweka jeshi la utawala huo haramu kwenye orodha yake nyeusi - inayojulikana pia kama orodha ya aibu - kwa kukiuka haki za watoto katika maeneo yenye migogoro, akidai kwamba jeshi la Israel ndilo "jeshi lenye maadili zaidi" na hakuna uamuzi wowote wa kulibadilisha hilo.
-
Sababu za uwezekano wa kutokea vita kati ya utawala wa Kizayuni na Hizbullah ya Lebanon
Jun 08, 2024 01:52Katika hali ambayo utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake ya kijeshi uliyoyatangaza katika vita dhidi ya Gaza, vyanzo vya habari vya Kizayuni vimeonya kuhusu harakati za baraza la mawaziri la utawala huo za kutaka kuingia katika vita vya pande zote na Hizbullah ya Lebanon.
-
Iran: Maafa ya Palestina hayataisha mpaka Marekani na Ulaya zitapoacha kuiunga mkono Israel
Jun 08, 2024 00:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Kusimamishwa kikamilifu na kivitendo uungaji mkono wa Marekani na Ulaya kwa utawala wa kibaguzi wa Kizayuni katika mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Ghaza ndiko kunakoweza kukomesha maafa machungu na ukatili wa kinyama na unaofanywa bila kujali dhidi ya watu huko Palestina.
-
Al Houthi: Jeshi la Yemen litaendelea kushambulia manowari kubwa ya kivita ya Marekani
Jun 07, 2024 08:49Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameapa kwamba Jeshi la nchi hiyo litaendelea kulenga meli kubwa ya kivita ya Marekani yenye uwezo wa kusheheni ndege za kivita ijulikanayo kama USS Dwight D. Eisenhower.
-
HAMAS yatoa vipigo vingine vikali kwa wanajeshi vamizi wa Israel
Jun 07, 2024 02:51Brigedi za Shahid Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa zimeendelea kuviwinda na kuvitwanga kwa makombora vifaru vya utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.
-
UNICEF: Kila watoto 9 kati ya 10 huko Ghaza wanakabiliwa na ukata wa kupindukia wa chakula
Jun 06, 2024 06:24Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeripoti kuwa, kati ya kila watoto 10, tisa kati yao wanateseka kwa ukata mkubwa wa chakula kutokana na utawala wa Kizayuni kuuzingira kila upande Ukanda wa Ghaza na kufunga vivuko vya mpakani.
-
Majibu ya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon dhidi ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni
Jun 06, 2024 06:23Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, imejibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni kwa kushambulia kwa makombora ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo katili huko Palestina.