UN yalaaani vikali kitendo kisicho cha kimaadili cha mwakilishi wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i112716-un_yalaaani_vikali_kitendo_kisicho_cha_kimaadili_cha_mwakilishi_wa_israel
Stéphane Dujarric, Msemaji Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali hatua isiyo ya kimaadili ya mwakilishi wa utawala wa Kizayuni baada ya umoja huo kuamua kuiweka Israel katika orodha ya madola yanayofanya uhalifu wa kivita na kuua watoto wadogo.
(last modified 2024-06-08T23:48:46+00:00 )
Jun 08, 2024 23:48 UTC
  • UN yalaaani vikali kitendo kisicho cha kimaadili cha mwakilishi wa Israel

Stéphane Dujarric, Msemaji Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali hatua isiyo ya kimaadili ya mwakilishi wa utawala wa Kizayuni baada ya umoja huo kuamua kuiweka Israel katika orodha ya madola yanayofanya uhalifu wa kivita na kuua watoto wadogo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dujarric amesema, kitendo cha Gilad Erdan, mwakilishi wa utawala wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa cha kusambaza mazungumzo ya sauti yaliyohusu kuwekwa Israel kwenye orodh nyeusi ya wavunjaji wa haki za binamu, ni kitendo kiovu kisichoendana na mtu mwenye hadhi ya kidiplomasia. 

Mkanda huo wa sauti ni ule ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaambia wawakilishi wa Israel kwenye umoja huo kwamba, atauweka utawala wa Kizayuni katika orodha ya madola yenayofanya jinai za kivita na kuua watoto wadogo. 

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Katika upande mwingine, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu amekasirishwa sana na hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuliweka jeshi la utawala huo haramu kwenye orodha yake nyeusi - inayojulikana pia kama orodha ya aibu - kwa kukiuka haki za watoto katika maeneo yenye migogoro, akidai kwamba jeshi la Israel eti ndilo "jeshi lenye maadili zaidi" na hakuna uamuzi wowote wa kulibadilisha hilo.

Zaidi ya Wapalestina 36,700 wameshauawa shahidi hadi sasa huko Ghaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo, na wengine zaidi ya 83,500 wamejeruhiwa katika mashambulio ya kikatili ya Israel.

Sehemu kubwa ya majengo ya ukanda huo yamegeuka magofu huku jeshi la Kizayuni likiendelea kuweka kizuizi cha kufikishwa chakula, maji safi na dawa kwa wakazi wa eneo hilo wanaoatilika kwa njaa.