-
Wanajeshi 14 wa Israel waangamizwa, wajeruhiwa katika operesheni ya muqawama Gaza
Apr 29, 2024 07:49Takriban wanajeshi watatu wa utawala katili wa Israel wameangamizwa na wengine 11 kujruhiwa vibaya katika eneo la vita kati kati mwa Ukanda wa Gaza, huku vikosi vya muqawama au mapambano ya Kiisalmu Palestina vikiendelea kulisababishia hasara kubwa jeshi katili la utawala huo.
-
UNRWA: Takriban watoto 17,000 wametenganishwa na familia zao Gaza kufuatia vita vya Israeli
Apr 29, 2024 07:33Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limebainisha wasiwasi wake juu ya hali inayozidi kuzorota ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, huku Israel ikiendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo linalozingirwa.
-
Rais wa Syria: Mshikamano wa nchi za Kiarabu unapelekea kupatikana utulivu katika eneo
Apr 28, 2024 23:36Rais wa Syria amesema kuwa kuwepo mshikamamo baina ya nchi za Kiarabu na kutekeleza hatua za pamoja kutapelekea kupatikana amani na uthabiti katika eneo.
-
Abbas: Utawala wa Kizayuni umeangamiza asilimia 75 ya Ukanda wa Gaza
Apr 28, 2024 23:07Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeangamiza asilimia 75 ya nyumba, miundombinu ya barabara, vyuo vikuu, misikiti na miundo msingi mingine ya Ukanda wa Gaza.
-
Viongozi wa makundi ya Palestina wakutana Istanbul, Uturuki kujadili yanayojiri Ghaza
Apr 28, 2024 08:23Viongozi wa Harakati za Hamas, Jihadul-Islami na Vuguvugu la Wananchi la Ukombozi wa Palestina wamekutana kujadili yanayojiri kwenye medani za mapambano na za kisiasa za Palestina na vita katika Ukanda wa Ghaza.
-
Uwezekano wa ICC kutoa waranti wa kukamatwa Netanyahu kwa mauaji ya Ghaza umeitia tafrani Israel
Apr 28, 2024 08:15Baraza la mawaziri la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limeingiwa na tafrani na wasi wasi mkubwa juu ya uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu na maafisa wengine waandamizi kwa kuhusika na jinai za vita vya miezi kadhaa vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza uliozingirwa.
-
Kushadidi mgogoro wa kisiasa katika baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni
Apr 28, 2024 07:22Kuendelea maandamano ya mitaani huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), tofauti za kimtazamo kati ya wapinzani na baraza la mawaziri na kuongezeka uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kutoa amri ya kumkamata Benjamin Netanyahu kumezidisha mzozo wa kisiasa huko Tel Aviv.
-
Wapalestina 37 wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel huko Gaza
Apr 28, 2024 03:50Wapalestina 37 wameuawa shahidi katika mashambulio ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel katikati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Amnesty International: Ubaguzi wa apartheid wa Israel dhidi ya Wapalestina hauwezi kukanushwa
Apr 28, 2024 00:57Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International amesema kuwa, utawala wa Israel umetekeleza ubaguzi wa apartheid dhidi ya Wapalestina. Agnes Callamard amesema kuwa, ameshangazwa mno na utumiaji mabavu wa kimfumo wa utawala ghasibu wa Israel.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Apr 28, 2024 00:56Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.