Apr 29, 2024 03:06 UTC
  • Rais wa Syria: Mshikamano wa nchi za Kiarabu unapelekea kupatikana utulivu katika eneo

Rais wa Syria amesema kuwa kuwepo mshikamamo baina ya nchi za Kiarabu na kutekeleza hatua za pamoja kutapelekea kupatikana amani na uthabiti katika eneo.

Rais Bashar al Assad wa Syria ameeleza haya jana katika mazungumzo na Abdullatif bin Rashid al Zayani Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain huko Damascus kuhusu kuanzisha uhusiano wa pande mbili  na njia ya kustaiwsha uhusiano huo. Pande mbili hizo aidha zimegusia kufanyika juhudi kwa ajili ya kufanyika mkuktano wa wakuu wa nchi za Kiarabu uliopangwa kufanyika mwezi ujao huko Manama mji mkuu wa Bahrain. 

Rais wa Syria na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain pia wamechunguza masuala muhimu yaliyoorodheshwa katika ajenda ya kazi ya mkutano ujao wa wakuu wa Kiarabu.  

Bahrain ni nchi ya pili ya Kiarabu ambayo imefungua  tena ubalozi wake mjini Damascus uliokuwa umefungwa baada ya kuanza mgogoro wa Syria mwaka 2011.  

Hatua ya sasa ya nchi za Kiarabu ya kuigeukia Syria; nchi ambazo zilihusika moja kwa moja kuibua mgogoro nchini humo ni ishara ya wazi ya kushindwa kwa mpango wa kuipindua serikali halali ya Syria na wakati huo huo ni ushindi wa kisiasa na kijeshi kwa Syria. 

 

Tags