-
Hizbullah yatekeleza mashambulizi ya mizinga na droni dhidi ya ngome za Israel
May 12, 2024 04:00Wapiganaji wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, wamefanya mashambulizi kadhaa ya kijeshi kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni) na mizinga dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Afisa wa Hamas: Muqawama wa Gaza umeweza kukabiliana kwa mafanikio na vita vya dunia
May 11, 2024 23:06Sami Abu Zuhri, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kwamba Muqawama na mapambano ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kukabiliana na "vita vya kimataifa," na nchi zilizoifadhili Israel sasa zinaanza kusitisha uungaji mkono wao kwa utawala huo.
-
Watu 200 wafariki dunia kwa janga la mafuriko nchini Afghanistan
May 11, 2024 08:04Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kwa akali watu 200 wamefariki duniani kwa mafuriko kaskazini mwa Afghanistan.
-
Askari wa Israel waendelea kuangamizwa na wanamuqawama Gaza
May 11, 2024 04:29Wanajeshi wengine watano wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa katika shambulizi la ulipizaji kisasi lililofanywa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS katika Ukanda wa Gaza.
-
Abdollahian: Iran iko tayari kushirikiana na Ulaya kwa kuzingatia maslahi ya pamoja
May 11, 2024 00:44Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kushirikiana na Ulaya kwa kuzingatia maslahi ya pande mbili.
-
Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yakwama, wajumbe wa Hamas na Israe waondoka Cairo
May 11, 2024 00:42Mazungumzo yaliyokuwa na lengo la kuhitimisha vita vya Gaza yaliyokuwa yakifanyika huko Cairo Misri yamekwama na pande mbili zimeshindwa kufikia makubaliano.
-
Njama za utawala wa Kizayuni za kuzusha mgogoro wa kibinadamu Rafah
May 10, 2024 07:26Katika kuendeleza jinai zake utawala wa Kizayuni umepanga kuzusha mgogoro wa kibinadamu huko Rafah.
-
Al Houthi: Yemen italenga meli zenye uhusiano na Israel bila kujali zinakoenda
May 10, 2024 06:40Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdul Malik al-Houthi, amesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vitalenga meli za kampuni yoyote inayohusiana na kusambaza au kusafirisha bidhaa hadi Israel bila kujali zinakoelekea.
-
Muqawama wa Iraq washambulia maeneo ya kistratajia ya Israel, Eilat
May 10, 2024 03:54Harakati ya Kiislamu ya Iraq imetangaza kuwa imeshambulia maeneo ya kistratajia ya Israel katika mji wa Eilat, ulioko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Yemen yashambulia meli 3 za Waisraeli katika Ghuba ya Aden, Bahari ya Hindi
May 09, 2024 22:39Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema vikosi vya jeshi la majini, anga na makombora vya nchi hiyo vimezishambulia meli tatu zenye uhusiano na Israel kama sehemu ya kampeni ya baharini ya kuwaunga mkono na kuwatetea Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.