-
Kashfa ya kutoweka raia 10,000 wa Palestina katika vita vya Gaza
May 03, 2024 23:00Sambamba na kuendelea kupanuka maandamano ya wanafunzi wa Marekani na juhudi za Mahakama ya ICJ na ICC za kutoa waranti wa kukamatwa viongozi wa utawala wa kibaguzi wa Israel kutokana na jinai zao huko Gaza, Shirika la Haki za Binadamu la Euro-Mediterranean limetoa ripoti mpya na ya kutisha inayoweza kuzidisha hasira za wanafunzi hao na wakati huo huo kuongeza ushahidi mpya katika jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina.
-
Ujenzi mpya wa Gaza waweza kuchukua miaka 80 kukamilika, kuna uharibifu ambao haujawahi kuonekana tangu Vita vya Dunia
May 03, 2024 07:05Afisa wa Umoja wa Mataifa anasema uharibifu uliosababishwa na vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haujawahi kuonekana tangu Vita vya Pili vya Dunia, huku akikadiria kuwa ujenzi mpya wa eneo hilo la Palestina unaweza kuchukua miaka 80 na kugharimu hadi dola bilioni 40.
-
Ansarullah ya Yemen: Mauaji ya kimbari imekuwa tabia ya kila siku ya Wazayuni
May 03, 2024 04:17Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameichukulia mienendo ya kila siku ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Uturuki yasitisha biashara na Israel kulalamikia maafa ya kibinadamu Gaza
May 03, 2024 03:53Serikali ya Uturuki imetangaza kuwa, imesitisha biashara zote na utawala ghasibu wa Israel kutokana na mashambulizi yake huko Gaza, ikitoa mfano wa "janga la kibinadamu linalozidi kuongezeka" katika ukanda huo.
-
Kukatwa kikamilifu uhusiano wa Colombia na utawala wa Kizayuni; kuendelea kutengwa Tel Aviv kimataifa
May 02, 2024 23:13Rais Gustavo Petro wa Colombia alisema siku ya Jumatano tarehe Mosi Mei katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kuwa kuanzia Alhamisi amekata kikamilifu uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni kwa sababu ya jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Baada ya uamuzi wa kihistoria wa Colombia; Hamas yataka mataifa yote kuvunja uhusiano na Israel
May 02, 2024 08:16Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imepongeza na kukaribisha kwa mikono miwili uamuzi wa Colombia wa kuvunja uhusiano wake na utawala haramu wa Israel.
-
Colombia yaamua kuvunja uhusiano na Israel kwa sababu ya mauaji ya kimbari ya Ghaza
May 01, 2024 23:55Colombia imeamua kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Utawala wa Kizayuni umewatia nguvuni mamia ya wafanyakazi wa Kipalestina
May 01, 2024 23:06Vyanzo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa Wazayuni maghasibu wamewatia mbaroni zaidi ya wafanyakazi elfu tano wa Kipalestina katika mwaka huu wa 2024 huku hali za kiafya za raia hao wa Kipalestina zikitajwa kuwa mbaya.
-
Jitihada za China za kuleta maridhiano ya kitaifa Palestina
May 01, 2024 23:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ametangaza kuwa kufuatia mkutano wa wawakilishi wa harakati za Palestina za Hamas na Fat'h mjini Beijing, pande mbili zimefikia makubaliano ya kujadili maridhiano ya kitaifa huko Palestina.
-
Congress ya Marekani inatumika kama ngao ya kumlinda Netanyahu
May 01, 2024 08:10Katika hali ambayo Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni lina wasiwasi mkubwa kuhusiana na uwezekano wa kutolewa waranti wa kukamatwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu na maafisa wengine wa utawala wa Kizayuni, tovuti ya habari ya Axios imeripoti kwamba wajumbe wa Congress wameionya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kuitaka isitoe vibali vya kutiwa nguvuni maafisa wa utawala wa Israel.