Mateka wa Kipalestina waongezeka pakubwa katika jela za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109966-mateka_wa_kipalestina_waongezeka_pakubwa_katika_jela_za_utawala_wa_kizayuni
Klabu ya Mateka wa Palestina imetangaza kuwa kuna ongezeko kubwa sana la mateka wa Kipalestina wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni bila ya kuhukumiwa.
(last modified 2024-03-27T08:50:37+00:00 )
Mar 27, 2024 08:50 UTC
  • Mateka wa Kipalestina waongezeka pakubwa katika jela za utawala wa Kizayuni

Klabu ya Mateka wa Palestina imetangaza kuwa kuna ongezeko kubwa sana la mateka wa Kipalestina wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni bila ya kuhukumiwa.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Klabu ya Mateka wa Palestina imetangaza kuwa tangu kuanza mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza Okktoba 7 mwaka jana hadi sasa idadi ya raia wa Palestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia watu 3,558. 

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, idadi ya mateka wa kike walioko katika magereza ya utawala wa Kizayuni bila ya kuhukumiwa pia imeongezeka zaidi ikilinganishwa na siku za nyuma na kufikia kesi 19. 

Mateka wa Kipalestina katika jela za utawala wa Kizayuni 

Utawala wa Kizayuni unawafungia jela Wapalestina bila ya kuwahukumu na bila ya kuwafungulia mashtaka. 

Utawala wa Kizayuni unatumia sera ya kuwatia mbaroni na kuwaweka kizuizini raia wa Palestina bila ya mashtaka mahususi na pasina kuwafikisha mahakamani, jambo linalowanyima raia hao haki ya kuwasiliana na mawakili wao ili kujua sababu za kukamatwa kwao.