-
Wapalestina walaani hatua ya mataifa ya Magharibi ya kusimamisha misaada ya fedha kwa UNRWA
Jan 28, 2024 04:02Maafisa waandamizi wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wamekosoa uamuzi wa karibu nchi kumi za Magharibi wa kusitisha misaada ya fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa Wapalestina UNRWA na kuzitaka nchi hizo zibadilishe haraka uamuzi wao huo ambao wamesema utasababisha hatari "kubwa".
-
Yemen: Tunao uwezo wa "kuzizamisha" meli za adui katika Bahari Nyekundu, ya Arabia na Mediterania
Jan 28, 2024 03:08Yemen, ambayo imekuwa ikizishambulia meli zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kuwahami na kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanaoandamwa na mashambulio ya kinyama ya utawala huo, imesema inao uwezo wa "kuzizamisha" meli za adui mahali popote katika Bahari Nyekundu, ya Arabia na Mediterania.
-
Katika usiku mmoja, Muqawama wa Kiislamu washambulia mara 4 vituo vya US Syria na Iraq
Jan 28, 2024 02:52Wapiganaji wa harakati za Muqawama wa Kiislamu za Iraq wamezishambulia mara nne katika usiku mmoja kambi za kijeshi za Marekani nchini humo na katika nchi jirani ya Syria.
-
Hizbullah yaonya itajibu vikali mashambulizi ya Israel
Jan 27, 2024 22:58Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utapanua mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, utapata jibu kali na la sawasaw kutoka kwa harakati hiyo.
-
Hukumu ya Mahakama ya The Hague; Nukta muhimu katika kutafuta haki kwa ajili ya watu wa Palestina
Jan 27, 2024 08:40Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, yenye makao yake huko The Hague Uholanzi imetoa hukumu yake ya awali kwa shauri la mashtaka lililowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji ya kimbari ya utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Makombora ya Hizbullah ya Lebanon yapiga ngome za kijeshi za Israel
Jan 27, 2024 08:33Wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wameshambulia kwa makombora vituo na ngome za kijeshi za Israel kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kusambaratisha mfumo wa kamera za usalama wa utawala huo haramu.
-
Israel yapuuza amri ya ICJ, yaendelea kumwaga damu za Wapalestina Gaza
Jan 27, 2024 08:22Utawala haramu wa Israel umedharau uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuutaka uchukue hatua zote zinazohitajika kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, na badala yake jeshi la utawala huo pandikizi limeendelea kumwaga damu za Wapalestina wa Gaza.
-
Yemen yaishambulia kwa makombora meli ya mafuta ya Uingereza katika Ghuba ya Aden
Jan 27, 2024 02:54Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limeishambulia kwa makombora meli ya mafuta ya Uingereza katika Ghuba ya Aden.
-
Wapalestina zaidi ya 26,000 wameuawa shahidi tangu Israel ianzishe mauaji ya kimbari Gaza
Jan 26, 2024 23:06Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na jeshi katili la Israel huko Gaza tangu Oktoba 7 imeongezeka na kufikia 26,083.
-
Maandamano makubwa ya kuunga mkono Gaza na muqawama yafanyika Yemen
Jan 26, 2024 07:41Maandamano makubwa ya Wayemeni ya kuunga mkono Gaza na kuidhinisha operesheni ya jeshi la Yemen dhidi ya uvamizi wa Marekani na Uingereza yamefanyika tena Ijumaa ya leo.