Maandamano makubwa ya kuunga mkono Gaza na muqawama yafanyika Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i107652-maandamano_makubwa_ya_kuunga_mkono_gaza_na_muqawama_yafanyika_yemen
Maandamano makubwa ya Wayemeni ya kuunga mkono Gaza na kuidhinisha operesheni ya jeshi la Yemen dhidi ya uvamizi wa Marekani na Uingereza yamefanyika tena Ijumaa ya leo.
(last modified 2024-01-26T07:41:57+00:00 )
Jan 26, 2024 07:41 UTC
  • Maandamano makubwa ya kuunga mkono Gaza na muqawama yafanyika Yemen

Maandamano makubwa ya Wayemeni ya kuunga mkono Gaza na kuidhinisha operesheni ya jeshi la Yemen dhidi ya uvamizi wa Marekani na Uingereza yamefanyika tena Ijumaa ya leo.

Maandamano hayo ya Wayemeni yamefanyika huko Saada na Rima kaskazini na magharibi mwa Yemen kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa Gaza na  wakati huo huo kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji wametangaza pia himaya na uungaji mkono wao kwa operesheni za kijeshi za Yemen za kukabiliana na uuvamizi wa Uingereza na Marekani. Taarifa zaidi zinasema maandamano ya leo yalifanyika kwa anuanii ya "Yemen na Palestina zipo katika kambi moja".

Waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na maberamu sambamba na bendera za Palestina na Yemen walisikika wakipiga nara za kulaani jinai za utawala haramu wa Israel huko Gaza. Aidha baadhi ya jumbe zilizokuwa zimeandikwa katika mabango hayo zilisomeka: "Tuko tayari kwa viita na Marekani", "Tumejiandaa kuiwinda Marekani", "Labbaiika ya Aqswa" na "Allah Akbar, Marekani shetani mkubwa.

 

Waandamanaji hao wa Yemen wamesisitiza kuwa: Jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina na mauaji ya umati, uchomaji moto kambi za wakimbizi na kulipuliwa majengo ni jinai za kivita, na adui Mzayuni na washirika wake wa kimataifa watahukumiwa kwa jinai hizo.

Wakati huo huo, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Abdul-Malik al-Houthi anasema kulengwa kwa meli zinazohusishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu kutaendelea hadi Wapalestina walioko Gaza watakapoweza kupokea misaada. Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Alhamisi, al-Houthi alisema sababu kuu hatua hiyo ni kuendelea jinai za Wazayuni ni msimamo wa Marekani wa kuunga mkono jinai hizo.