-
Tangazo la Marekani la kuwa tayari kwa mazungumzo ya kuhitimisha kuwepo kwake kijeshi nchini Iraq
Jan 26, 2024 04:27Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, katika barua ambayo balozi wa Marekani mjini Baghdad, Alina Romanovsky aliiwasilisha siku ya Jumatano kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hossein, Washington imetangaza kuwa iko tayari kuanza mazungumzo na Baghdad ya kuhitimisha uwepo kijeshi wa nchi hiyo na washirika wake katika ardhi ya Iraq.
-
Al-Houthi: Kulenga meli zinazohusishwa na Israel katika Bahari Nyekundu kutaendelea
Jan 25, 2024 23:49Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Abdul-Malik al-Houthi anasema kulengwa kwa meli zinazohusishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu kutaendelea hadi Wapalestina walioko Gaza watakapoweza kupokea misaada.
-
Ansarullah yaitaka UN iwaondoe Yemen wafanyakazi wake raia wa US, UK
Jan 25, 2024 07:42Harakati ya Ansarullah imeziagiza Marekani na Uingereza ziwaondoea nchini Yemen raia wake wanaoufanyia kazi Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Sana'a.
-
Ansarullah wakabiliana na manowari za Marekani, wapiga moja katika Bahari Nyekundu
Jan 25, 2024 04:34Wapiganaji wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen wametangaza kuwa wamepiga meli ya kivita ya Marekani na kulazimisha meli nyingine mbili za kibiashara za nchi hiyo kurudi kusini mwa Bahari Nyekundu, katika shambulio la hivi karibuni zaidi la harakati hiyo katika eneo hilo lenye umuhimu wa kimkakati.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway: Hali ya Gaza ni sawa na Jahanamu ya duniani
Jan 25, 2024 04:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway amekemea mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na hali mbaya ya Ukanda wa Gaza katika nyanja zote za kibinadamu na kijamii na kusema: "Hali ya hivi sasa katika eneo hilo ni sawa na Jahanamu ya duniani."
-
Baghdad yalaani mashambulizi ya makombora ya Marekani dhidi ya Iraq
Jan 24, 2024 23:57Msemaji wa Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iraq amelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya vituo na ngome za Jeshi la Iraq na makundi ya muqawama yanayopambana na ugaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
WHO yatoa wito wa kukomeshwa "hali inayoshabihiana na Jahannam" katika Ukanda wa Gaza
Jan 24, 2024 09:32Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kukomeshwa hali inayofanana na moto wa Jahannam inayowakumba raia na wafanyakazi wa afya katika Ukanda wa Gaza.
-
Ghaza imeendelea kuwa makaburi ya halaiki ya wanajeshi vamizi wa Israel + VIDEO
Jan 24, 2024 03:27Izzat al-Rishq, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, ukanda wa Ghaza utaendelea kuwa makaburi ya halaiki ya wanajeshi wa Israel waliouvamia ukanda huo na kwamba mfano wa wazi ni kuangamizwa wanajeshi 24 wa utawala wa Kizayuni kwa mkupuo mmoja siku chache zilizopita.
-
Netanyahu: Tumepata pigo kubwa baada ya wanajeshi weu 24 kuuawa kwa siku moja
Jan 24, 2024 00:32Baada ya wanajeshi 24 wa utawala ghasibu wa Israel kuangamizwa huko Gaza, Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu amesema kuwa, hilo ni pigo kubwa zaidi kwa Israel tangu kuanza vita hivyo.
-
UN: Utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia njaa kama 'silaha' dhidi ya Wapalestina
Jan 23, 2024 09:51Ripota wa Umoja wa Mataifa anasema utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia njaa kama silaha dhidi ya watu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula baada ya miaka ya vikwazo na vita vya sasa vya maangamizi ya umati vinavyotekelezwa na Israel.