-
Palestina: Kwa siku 108, Israel imeua watoto 11,000 na wanawake 7,500 Gaza
Jan 23, 2024 03:08Mamlaka za Palestina zimetangaza kuwa, jeshi vamizi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeua watoto 11,000 na wanawake 7,500 katika Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa jeshi hilo katili limedondosha zaidi ya tani 65,000 za mada za miripuko katika vita vya upande mmoja lilivyoanzisha dhidi ya Wapalestina waliowekewa mzingiro.
-
Axios: Israel imependekeza kwa HAMAS mpango mpya wa kubadilishana mateka
Jan 23, 2024 02:29Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umependekeza kwa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS mpango mpya wa kubadilishana mateka kupitia "usitishaji" mapigano kwa muda wa hadi siku 60 ili mateka wote waliosalia, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo, waweze kuachiwa.
-
HAMAS: Wapalestina 500,000 wa Gaza wapo katika hatari ya kufa njaa
Jan 22, 2024 23:40Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema zaidi ya watu nusu milioni wakazi wa Ukanda wa Gaza wapo katika hatari ya kufa njaa kutokana na taathira hasi za vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo lililozingirwa.
-
Kupungua pakubwa uungaji mkono kwa utawala wa Kizayuni duniani
Jan 22, 2024 22:42Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Morning Consult yanaonyesha kuwa uungaji mkono wa kimataifa kwa utawala wa Kizayuni umepungua sana kufuatia vita vilivyoanzishwa na utawala huo haramu dhidi ya wakazi wa Palestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Walimwengu waendelea kutoa mwito wa kuwepo taifa huru la Palestina
Jan 22, 2024 09:48Viongozi mbalimbali wa dunia wametoa miito ya usitishwaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuwepo kwa suluhisho la mataifa mawili ya Israel na Palestina na kusema kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuwepo amani ya kudumu eneo hilo.
-
Hujuma za Israel zimebomoa misikiti 1,000 Gaza tokea Oktoba 7
Jan 22, 2024 08:32Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini katika Ukanda wa Gaza imesema mashambulizi ya vikosi vya utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo lililozingirwa yamebomoa na kuharibu misikiti 1,000 tokea Oktoba 7 mwaka uliopita hadi sasa.
-
Mufti wa Oman: Kujitahidi kwa Ukombozi wa Al-Aqsa ni wajibu kwa Waislamu wote
Jan 22, 2024 04:01Mufti Mkuu wa Oman kwa mara nyingine amesisitiza umuhimu wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel na akasema kuukomboa ni jukumu la Waislamu wote duniani.
-
Israel inaiangamiza Palestina kielimu kwa kulenga wasomi na vituo vya kielimu Gaza
Jan 22, 2024 04:00Utawala wa Kizayuni wa Israel umewauwa maprofesa 94 wa vyuo vikuu, mamia ya walimu, na maelfu ya wanafunzi katika Ukanda wa Gaza katika muda wa miezi mitatu, kwa mujibu wa shirika moja huru la kutetea haki za binadamu.
-
Hizbullah yazima uvamizi wa kijeshi wa Israel kusini ya Lebanon
Jan 22, 2024 03:59Wanajihadi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wametibua uvamizi wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu, huku ngome za utawala huo ghasibu zikiendelea kulengwa kwa makombora ya kundi hilo la muqawama, likiwa ni jibu kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS: Shambulio la Oktoba 7 ilikuwa "hatua ya lazima" dhidi ya ukaliaji ardhi kwa mabavu wa Israel
Jan 22, 2024 00:17Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, shambulio la tarehe 7 Oktoba 2024 dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel lilikuwa "hatua ya lazima" dhidi ya ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na utawala huo dhalimu katika maeneo ya Palestina.