-
Wazayuni washangazwa na uwezo mkubwa wa HAMAS wa kuzalisha silaha
Jan 21, 2024 23:29Utawala wa Kizayuni umelazimika kukiri kuwa umeshangazwa sana na jinsi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilivyo na uwezo mkubwa wa kuzalisha silaha ndani ya Ukanda wa Ghaza ambao umezingiwa kila upande kwa miaka mingi.
-
Mapendekezo ya Iran kwa ajili ya amani ya kudumu huko Palestina yawasilishwa NAM
Jan 21, 2024 23:27Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Mokhber, amewasilisha mapendekezo ya Iran kwa ajili ya kutatua suala la Palestina katika mkutano wa 19 wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) unaofanyika Kampala, nchini Uganda.
-
Waliouawa shahidi Gaza wapindukia 25,000, Israel yaendeleza mashambulizi ya kinyama
Jan 21, 2024 10:09Maafisa wa Palestina katika Ukanda wa Gaza wametangaza kuwa, wakati vita angamizi vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza vimeingia katika siku yake ya 107 leo, hadi sasa Wapalestina 25,105 wameshauawa shahidi na 62,681 wamejeruhiwa.
-
Marekani: Israel imeshindwa kufikia lengo la vita, HAMAS ingali iko imara, ina silaha za kutosha
Jan 21, 2024 09:18Mashirika ya intelijensia ya Marekani yamesema, idadi ya vifo vya wapiganaji wa harakati ya HAMAS vilivyotokana na uvamizi unaoendelea wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haifikii lengo la utawala huo la kulitokomeza kundi hilo la muqawama wa Palestina.
-
Wanamuqawama wa Iraq wakishambulia kituo cha jeshi la Marekani kwa maroketi na makombora 40
Jan 21, 2024 07:56Vikosi vya Muqawama wa Iraq vimekishambulia kwa maroketi na makombora 40 kituo cha wanajeshi vamizi wa Marekani cha A'inul-Assad kilichoko kwenye mkoa wa Al-Anbar.
-
Mapigano makali kati ya wanamuqawama wa Palestina na wanajeshi wa Kizayuni magharibi mwa Gaza
Jan 21, 2024 04:13Vyombo vya habari vya Palestina leo Jumapili vimeripoti mapigano makali kati ya vikosi vya makundi ya muqawama na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel magharibi mwa mji wa Gaza.
-
Sayyid Nasrullah: Gaza ni nembo ya umoja wa damu, silaha, medani na lengo la Umma wa Kiislamu
Jan 20, 2024 23:10Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah ametuma ujumbe katika Mkutano wa 12 wa Kimataifa wa "Gaza; Nembo ya Muqawama" na kusisitiza kuwa Gaza leo hii ni nembo ya umoja wa damu, silaha, medani na lengo la Umma wa Kiislamu.
-
Dunia yaendelea kupinga matamshi ya Netanyahu kuhusu taifa la Palestina
Jan 20, 2024 07:09Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wameendelea kupinga na kukemea matamshi yalitotolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akipinga suala la kutambuliwa rasmi taifa huru la Palestina.
-
Vita vya Gaza na kuongezeka changamoto ndani ya utawala wa Kizayuni
Jan 20, 2024 04:45Kuendelea vita vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza kumezidisha changamoto ndani ya utawala huo ghasibu.
-
UN: Maelfu ya Wapalestina wa Gaza waliokamatwa na askari wa Israel wanateswa
Jan 20, 2024 03:52Umoja wa Mataifa umesema huenda vikosi vya jeshi la Israel vimewakamata maelfu ya Wapalestina wakazi wa Ukanda wa Gaza, huku utawala huo wa Kizayuni ukiendeleza mauaji na jinai za kutisha dhidi ya wakazi wa eneo hilo uliolizingira.