Wazayuni washangazwa na uwezo mkubwa wa HAMAS wa kuzalisha silaha
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i107484-wazayuni_washangazwa_na_uwezo_mkubwa_wa_hamas_wa_kuzalisha_silaha
Utawala wa Kizayuni umelazimika kukiri kuwa umeshangazwa sana na jinsi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilivyo na uwezo mkubwa wa kuzalisha silaha ndani ya Ukanda wa Ghaza ambao umezingiwa kila upande kwa miaka mingi.
(last modified 2024-01-21T23:29:02+00:00 )
Jan 21, 2024 23:29 UTC
  • Wazayuni washangazwa na uwezo mkubwa wa HAMAS wa kuzalisha silaha

Utawala wa Kizayuni umelazimika kukiri kuwa umeshangazwa sana na jinsi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilivyo na uwezo mkubwa wa kuzalisha silaha ndani ya Ukanda wa Ghaza ambao umezingiwa kila upande kwa miaka mingi.

Gazeti la Kizayuni la Maariv limetoa ripoti maalumu kuhusu suala hilo na kuwanukuu wataalamu wa utawala wa Kizayuuni wakishindwa kuficha mshangao wao mkubwa juu ya namna HAMAS inavyoweza kuzalisha silaha kubwakubwa ndani ya Ukanda wa Ghaza.

Alon Ben-David, mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Israel amesisitiza kuwa,  brigedi ya 98 ya jeshi la Israel karibu hivi itatangaza kumalizika operesheni zake huko Khan Yunus, kusini mwa Ukanda wa Ghaza wakati ambapo hadi hivi sasa inatamani kupata japo kitu kimoja cha kukiita ni ushindi wake kwenye operesheni hizo.

Silaha za HAMAS ni jinamizi kwa Israel

 

Mtaalamu huyo wa masuala ya kijeshi wa utawala wa Kizayuni ameongeza kuwa, licha ya kupita zaidi ya miezi mitatu tangu Israel ilipoanzisha vita huko Ghaza lakini bado Israel imeshindwa kujua walipo viongozi wa HAMAS kama ambavyo pia imeshindwa kukomboa mateka wa utawala wa Kizayuni kutoka mikononi mwa HAMAS.

Amesema, watu wengi wanakosea wanapodhani kuwa silaha za HAMAS zinaingizwa kwa magendo kwenye Ukanda wa Ghaza kupitia mpaka wa Misri kwani ukweli ni kuwa asilimia kubwa sana ya silaha wanazotumia wanamapambano wa Palestina zinazalishwa ndani ya ukanda huo na ni kiwango kidogo mno kinachoingizwa kwa magendo kutoke nje ya eneo hilo.

Ben-David pia amesma, sasa hivi HAMAS ina uwezo mkubwa wa kuzalisha silaha mpya na zenye nguvu kubwa zaidi na kuzifanyia majaribio kwa kuwapiga wanajeshi wa Israel.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kijeshi wa utawala wa Kizayuni amekiri pia kwamba wanamapambano wa Palesina wamepata mafunzo makubwa zaidi ya kijeshi kuliko yale yanayotolewa ndani ya Israel.