-
Wazayuni wakiri kuwa Marekani inashiriki kivitendo katika mauaji ya watu wa Gaza
Dec 07, 2023 01:31Wizara ya Vita ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imekiri katika taarifa kwamba utawala huo umepokea tani 10,000 za zana za kivita kutoka Marekani tangu ulipoanzisha vita dhidi ya watu wa Gaza mnamo tarehe 10 Oktoba.
-
Hamas ina mpango kabambe wa kujihami katika vita na Israel
Dec 06, 2023 08:51Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya Palestina, Hamas, amesema harakati hiyo ya kupigania ukombozi wa Palestina yenye makao yake Gaza imeandaa mpango mkubwa wa kujihami katika kukabiliana na mashambulizi ya Israel, na kusisitiza kwamba umoja kati ya makundi ya muqawama wakati wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa uliwashangaza makamanda wa kijeshi wa Israel.
-
UNRWA: Gaza imekuwa 'mojawapo ya maeneo hatari zaidi' duniani
Dec 06, 2023 08:29Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) leo Jumatano limesema kuwa Ukanda wa Gaza sasa ni "mojawapo ya maeneo hatari zaidi" duniani, huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mashambulizi na mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo la Palestina linalozingirwa.
-
Israel kuanzisha tena vita kwailazimisha Yemen kuchukua hatua
Dec 06, 2023 05:30Hatua ya baraza la mawaziri lenye misimamo mikali la Netanyahu kukataa kukubali usitishaji vita wa kudumu kumeigharimu pakubwa Israel sio tu katika kuongeza vifo vya wanajeshi wake katika vita vya nchi kavu, bali pia katika kufungua tena pande mpya za vita dhidi ya utawala huo wa kibaguzi kutoka kusini mwa Lebanon hadi Golan ya Syria na Yemen.
-
Hamas: Madai yasiyo na msingi ya Biden ni kielelezo cha kuporomoka kwake kimaadili
Dec 06, 2023 04:42Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa, madai yasiyo na msingi ya Rais wa Marekani kuhusu operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa yanaonyesha kuporomoka kwake kimaadili.
-
Kanisa Palestina latumia magofu badala ya Mti wa Krismasi, lasema hakuna sherehe
Dec 05, 2023 23:33Kanisa moja la Palestina limeamua kuweka magofu ya nyumba zilizobomolewa badala ya Mti wa Krismasi kama ilivyo ada na kusema kuwa hakuna cha kusherehekea wakati huu utawala haramu wa Israel unapoendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Israel yadondosha mabomu ya fosforasi Khan Yunus huku ikiendeleza jinai Gaza
Dec 05, 2023 23:32Huku mashambulizi ya kikatili ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza yakiendelea, maafisa wa Palestina wanasema ndege za kivita za utawala huo zimelenga maeneo ya karibu na mji wa Khan Yunus kwa kutumia mabomu ya fosforasi ambayo yamepigwa marufuku na sheria za kimataifa.
-
Hamas: Kuendelea uwongo wa Israel; ni katika kukata tamaa ili kuchafua sura ya muqawama
Dec 05, 2023 08:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani hatua ya vyombo vya habari vya Magharibi ya kutangaza uwongo wa utawala wa Kizayuni kuhusu vita vya Gaza.
-
Israel yashambulia kwa mabomu shule 2 Gaza, 50 wauawa shahidi
Dec 05, 2023 03:24Vikosi vya utawala haramu wa Israel vimeshambulia kwa mabomu shule mbili katika Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina.
-
Mashirika ya haki Palestina yaonya kuhusu 'Nakba ya Pili' Gaza
Dec 05, 2023 03:22Mashirika matatu ya kutetea haki za binadamu ya Palestina yameashiria hatua ya Israel ya kuwafukuza kwa umati Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa, utawala huo wa Kizayuni unapanga kukariri Nakba ya pili katika eneo hilo lililozingirwa.