-
Wakuu wa Hizbullah, Jihad Islami wanakutana nchini Lebanon kuratibu mapambano dhidi ya Israel
Mar 20, 2023 00:54Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyed Hassan Nasrallah, na Mkuu wa Harakati Jihad Islami ya Palestina Ziyad Nakhalah wamejadili juu ya ushirikiano kati ya harakati hizo mbili za mapambano ya Kiislamu katika kukakbiliana na utawala haramu wa Israel na pia wamezungumza kuhusu matukio ya hivi punde katika Asia Magharibi.
-
Wapalestina waanzisha kampeni ya kuusafisha msikiti wa al-Aqsa kuukaribisha mwezi wa Ramadhani
Mar 19, 2023 09:16Mamia ya Wapalestina wakazi wa mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu wameanzisha kampeni ya kuusafisha Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa sambamba na kukaribia mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Syria: Kuchomwa Qur'ani nchini Ukraine kumefanyika kwa lengo la kugeuza vita vya kisiasa kuwa vya kidini
Mar 19, 2023 02:59Wizara ya Wakfu ya Syria imelaani vikali kitendo cha kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Ukraine, na kutangaza kwamba hatua hiyo imetekelezwa kwa lengo la "kugeuza vita vya kisiasa kuwa vita vya kidini".
-
Muungano wa al Fatah: Marekani haitaki ISIS itokomezwe nchini Iraq
Mar 19, 2023 02:45Mmoja wa viongozi wa Muungano wa al-Fath nchini Iraq ametangaza kuwa Marekani haitaki kuona kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) likiangamizwa kikamilifu nchini Iraq.
-
Kuuliwa shahidi Wapalestina 88 katika muda wa chini ya miezi 3
Mar 18, 2023 22:50Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni wamewaua shahidi Wapalestina 88 tangu kuanza mwaka huu wa 2023 hadi sasa.
-
OIC yaitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua kukabiliana na unyama wa Israel huko Palestina
Mar 18, 2023 22:45Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana kwa ajili ya kukabilina na hatua mbalimbali zisizo za kibinadamu za utawala haramu wa Israel huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu
-
Makundi ya mapambano ya Palestina: Wapalestina wasishiriki mkutano wa Sharm El-Sheikh
Mar 18, 2023 22:44Vyama na makundi ya mapambano ya Palestina yamemtaka Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuzuia ushiriki wa Wapalestina katika mkutano wa usalama wa Sharm El-Sheikh.
-
Morocco yasisitiza kuunga mkono kadhia ya Palestina
Mar 18, 2023 10:00Serikali ya Morocco imetangaza kuwa, inaunga mkono na kuipa umuhimu kadhia ya Palestina na kwamba, inalitazama syuala hilo kama moja ya mambo muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC wapongeza mapatano ya Iran na Saudia
Mar 18, 2023 04:36Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wamepongeza makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Saudi Arabia ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia.
-
Mufti wa Oman: Mapatano ya Iran na Saudia yameutia hofu na kiwewe utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 18, 2023 00:37Mufti wa Oman Sheikh Ahmad bin Hamad Al-Khalili amesisitiza haja ya kudumishwa amani na utangamano katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kubainisha kwamba, makubaliano na mapatano yaliyofikiwa kati ya Iran na Saudi Arabia yameutia hofu na kiwewe utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.