-
Katibu Mkuu wa Hizbullah amsifu Jenerali Soleimani kama ‘Kiongozi Mkuu’ katika mapambano dhidi ya Daesh na Israel
Jan 18, 2023 03:09Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amepongeza kujitolea mhanga kwa Luteni Jenerali Qassem Soleimani, akisema kamanda huyo mashuhuri alikuwa "Kiongozi Mkuu" aliyelishinda kundi la kigaidi la Daesh na kuuzuia utawala wa kigaidi wa Israel kuendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na Walebanon.
-
Syria yalaani vikwazo vya kikatili vya US dhidi ya sekta ya afya ya nchi hiyo
Jan 17, 2023 09:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeilaani vikali Marekani kwa kulenga sekta ya afya ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa vikwazo vya upande mmoja.
-
'Kufanyika kikao cha Kizayuni Azerbaijan ni utangulizi wa mapatano baina ya Baku na Tel Aviv'
Jan 17, 2023 03:53Makundi ya Muqawama ya Palestina yametangaza kuwa, kufanyika mkutano wa Wazayuni nchini Azerbaijan ni utangulizi wa kufikiwa mapatano baina ya Baku na Tel Aviv.
-
Ukurasa mwingine wa maafa ya binadamu huko Yemen; wagonjwa elfu tano wanaohitaji huduma ya Dialysis wanakaribia kuaga dunia
Jan 16, 2023 23:21Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen Anayehusika na Masula ya Tiba ameeleza kuwa maisha ya wagonjwa elfu tano wenye matatizo ya figo wako kwenye hatari ya kifo na Umoja wa mataifa na jamii ya kimataifa ndizo zinazopaswa kubeba dhima ya uhai na maisha ya raia hao wa Yemen.
-
Maandamano ya mapema dhidi ya serikali ya Netanyahu; indhari kuhusu vita vya ndani
Jan 16, 2023 04:46Makumi ya maelfu ya wakazi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) wameandamana kulalamikia maamuzi yaliyochukuliwa na serikali ya Benjamin Netanyahu ya kubana mfumo wa mahakama wa utawala huo.
-
Utawala wa Saudia wamhukumu kifo profesa wa chuo kikuu kwa kuiunga mkono Ikhwanul Muslimin
Jan 15, 2023 23:41Utawala wa Saudi Arabia umemhukumu kifo Profesa maarufu wa Chuo Kikuu kwa kutumia mitandao ya kijamii ya Twitter na WhatsApp kuliunga mkono kundi la Ikhwanul Muslimin na kusambaza habari zinazodaiwa kuwa za uhasama dhidi ya ufalme huo wa Aal Saud unaowakandamiza wapinzani na wanaharakati wa mageuzi nchini humo.
-
Mufti wa Oman: Njama ya Wazayuni ya kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa ni sawa na kutangaza vita
Jan 15, 2023 07:31Mufti wa Oman Shekhe Ahmed bin Hamad al-Khalili amesema, mwenendo ulioanzishwa na baraza la mawaziri la utawala haramu wa Kizayuni lenye misimamo ya kufurutu ada wa kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa unamaanisha kutangaza vita dhidi ya Umma wa Kiislamu.
-
Amir Abdollahian: Palestina ni suala la kwanza la ulimwengu wa Kiislamu
Jan 15, 2023 04:13Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao na kundi la viongozi na wanachama mashuhuri wa makundi mbalimbali ya mapambano ya Palestina kwamba Palestina na Quds Tukufu bado ni suala la kwanza la ulimwengu wa Kiislamu.
-
Mufti wa Masuni Iraq: Jinai dhidi ya makamanda wa muqawama inalazimu kulaaniwa Marekani
Jan 14, 2023 22:54Mufti wa Waislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq amelaani vikali jinai ya utawala wa Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani na Abu-Mahdi al-Mohandes na kueleza kuwa, jinai hiyo inalazimu Marekani kulaaniwa kila upande na kuchukuuliwa hatua.
-
Sababu za umuhimu wa safari ya Amir-Abdollahian nchini Lebanon
Jan 14, 2023 22:52Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Abdallah Bou Habib, Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Lebanon katika safari yake mjini Beirut na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima itaendelea kuwa rafiki mwaminifu na wa kutegemewa wa Lebanon.