-
Msemaji wa Hamas: Utawala wa Kizayuni unafuatiliwa usiku na mchana
Jan 12, 2023 00:51Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa mapambano ya kulinda na kuutetea msikiti wa al Aqsa na mateka wa Kipalestina yatakuwa ya aina yake na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unawajibika kubeba dhima ya matokeo ya hatua za kichochezi za Ben Gvir.
-
Kushadidi kukosolewa baraza la mawaziri lenye utata la Netanyahu
Jan 12, 2023 00:32Katika kipindi cha chini ya wiki mbili tokea lianze kazi baraza la mawaziri la serikali mpya ya utawala wa Kizayuni wa Israel inayoongozwa na Benjamin Netanyahu, ukosoaji dhidi ya baraza hilo umeshadidi kwa kiasi kikubwa na hata baadhi wameonya kuhusu uwezekano wa kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe katika utawala huo.
-
Hizbullah yailaani Charlie Hebdo kwa kumvunjia heshima Kiongozi Muadhamu
Jan 11, 2023 07:52Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali kitendo cha jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo cha kumvunjia heshima Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC yataka Mzayuni Ben-Gvir awekewe vikwazo
Jan 11, 2023 03:12Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitisha kikao cha dharura cha kuchunguza kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa na Wazayuni wenye itikadi kali. Kikao hicho kimefanyika mjini Jeddah Saudi Arabia na kusisitiza kuwekewa vikwazo waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni.
-
Ujumbe wa ngazi za juu wa Oman wawasili Sana'a, Yemen
Jan 10, 2023 23:46Duru za habari za Sana'a mji mkuu wa Yemen zimeripoti kuwa ujumbe wa ngazi ya juu wa Oman umewasili mjini humo kufuatilia suala la kurefushwa usitishaji vita nchini Yemen.
-
Imarati yajikomba zaidi kwa Israel, shule za nchi hiyo kufunza 'Holocaust'
Jan 10, 2023 03:47Umoja wa Falme za Kiarabu unaendelea kujidhalilisha na kujipendekeza kwa utawala haramu wa Israel, na sasa shule za nchi hiyo zinazatamiwa kuanza kufundisha 'ngano ya Holocaust' yaani mauaji ya halaiki ya Wayahudi yanayodaiwa kufanywa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani chini ya uongozi wa Adolf Hitler.
-
Biashara ya bidhaa za Iran yazidi kunawiri nchini Saudi Arabia
Jan 09, 2023 22:59Usafirishaji nje wa bidhaa za Iran kuelekea nchini Saudi Arabia umestawi hivi sasa baada ya kuanza mazungumzo baina ya nchi hizi mbili za Waislamu. Hayo yametokea baada ya biashara baina ya pande mbili kuzorota kwa miaka kadhaa.
-
Matukio muhimu sana na ya kuamua hatima kuhusiana na vita vya Yemen
Jan 09, 2023 22:57Matukio mawili mapya yamejiri kuhusiana na vita vya Yemen, ambayo kila moja ni muhimu na lina taathira kubwa ya kuamua hatima ya vita hivyo.
-
Mazungumzo ya Mawaziri wa Ulinzi wa Imarati na Syria mjini Damascus yaikasirisha Washington
Jan 09, 2023 08:06Washington imetoa radiamali kufuatia ziara ya karibuni ya Waziri wa Ulinzi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mjini Damascus na kutishia kuwa, hatua yoyote ya Imarati kuhuisha uhusiano na serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria itazigharimu pande mbili hizo.
-
OIC yaitisha kikao cha dharura kujadili hujuma za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa
Jan 09, 2023 04:17Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetangaza kuwa, wiki hii itaitisha kikao cha dharura cha nchi wanachama kwa ajili ya kujadili hujuma za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa.