-
Kuendelea kukandamizwa wanawake nchini Saudi Arabia
Jan 09, 2023 00:38Wanaharakati 35 wa kike wa Saudi Arabia wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela ikiwa ni muendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na ukoo wa Aal Saud dhidi ya wanawake.
-
"Walimwengu wamekuwa watazamaji tu wa jinai za Saudia dhidi ya Wayamen"
Jan 08, 2023 08:37Kituo cha Haki za Binadamu cha Yemen cha Ainu Yemen (Jicho la Yemen) kimetoa radiamali yake kuhusiana na jinai mpya za muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa Saudi Arabia na kutangaza kuwa, jamii ya kimataifa imeamua kuwa mtazamaji tu wa jinai zinazofanywa na Aal Saud na washirika wake huko nchini Yemen.
-
Maelfu waandamana katika ardhi za Palestina dhidi ya Waziri fisadi Netanyahu na serikali yake
Jan 08, 2023 03:50Maelfu ya wakazi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) wameandamana kupinga baraza jipya la mawaziri la Waziri Mkuu wa Israel lenye misimamo mikali. Baraza hilo jipya la Benjamin Netanyahu linatabiriwa kuanzisha sera hatari huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Kutolewa hukumu ya kumtia nguvuni Trump; Azma ya Iran na Iraq kwa ajili ya kuadhibiwa wahusika wa mauaji ya makamanda wa muqawama
Jan 07, 2023 22:51Sayyid Razi Imadi Faiq Zaidan, Mkuu wa Baraza Kuu la Mahakama la Iraq ameeleza kuwa chombo cha mahakama cha nchi hiyo kimetoa hukumu ya kutiwa mbaroni Donald Trump rais wa zamani wa Marekani ambaye amekiri hadharani kutekeleza jinai hiyo ya mauaji dhidi ya makamanda wa ushindi.
-
Nchi 14 za Kiarabu zinapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel
Jan 07, 2023 03:52Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa katika nchi 14 za Kiarabu yanaonesha kuwa, akthari ya watu wa nchi hizo wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Mwanazuoni wa Bahrain: Ni haramu kuwauzia ardhi Mayahudi
Jan 07, 2023 03:40Imamu Sala ya Ijumaa katika mji wa Al-Diraz nchini Bahrain, amesema kuwauzia ardhi Wayahudi ni sawa na kuiuza nchi na ni haramu.
-
Wayemen waandamana kitaifa dhidi ya muungano vamizi wa Saudia-Marekani
Jan 06, 2023 23:09Jana Ijumaa, wananchi wa Yemen walifanya maandamano makubwa katika mikoa mbalimbali kulaani uvamizi wa muungano wa Saudia na Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu na kuendelea kuzingirwa kila upande nchi yao pamoja na vitendo mbalimbali vya kuchochea vita vinavyofanya na madola vamizi.
-
Wasiwasi wa kieneo na kimataifa kuhusu tabia ya ubaguzi wa rangi ya baraza jipya la mawaziri la Israel dhidi ya Wapalestina
Jan 06, 2023 23:07Hatua ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa utawala haramu wa Israel, ya kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa imekabiliwa na radiamali kali ya kieneo na kimataifa, na ambayo imezipelekea nchi za China na Imarati kuomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadiliwa suala hilo.
-
Marekani ilikiuka mamlaka ya kujitawala Iraq kwa kuwaua Jenerali Soleimani na Al Muhandis
Jan 06, 2023 06:25Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani amemuenzi kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad miaka mitatu iliyopita, na kusema kuwa mauaji hayo yalikuwa "shambulio kali" dhidi ya uhuru na mamlaka ya kujitawala Iraq.
-
Kuongezeka umaarufu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani duniani, hasa barani Asia
Jan 06, 2023 04:20Sambamba na kuadhimishwa mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes, habari na ripoti zilizochapishwa kuhusu kufanyika sherehe katika maeneo mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa uungwaji mkono na umaarufu wa jenerali huyo mashuhuri umeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na hasa miongoni mwa vijana.