-
Pigo jingine kwa Wazayuni, Morocco yasherehekea kwa bendera ya Palestina, kupanda Kombe la Dunia + Video
Dec 02, 2022 04:31Katika hali ambayo serikali ya Morocco imetangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu na ya Waislamu, wamezidi kuonesha kutokubaliana na uamuzii huo wa utawala wa kifalme wa Morocco.
-
Wamorocco washerehekea ushindi Kombe la Dunia kwa kuiunga mkono Palestina
Dec 02, 2022 04:25Mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Morocco wamesikika wakipiga nara na kaulimbiu za kuiunga mkono Palestina baada ya timu yao kufuzu kuingia hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Dunia la 2022 zinazofanyika nchini Qatar.
-
Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili
Dec 02, 2022 04:24Mwandishi wa habari na mpinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amekosoa kufanyika tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST katika ardhi ya maeneo mawili matakatifu (Haramaini-Sharifaini) ya Makka na Madina na kueleza kwamba: Bin Salman anatoa huduma kubwa zaidi kwa maadui wa Uislamu kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa kufanyia ufisadi wa kimaadili.
-
Sisitizo la Pakistan la kuendelea na misimamo yake dhidi ya Israel
Dec 01, 2022 23:12Waziri Mkuu wa Pakistan Muhammad Shahbaz Sharif ameitaja hali ya kutia wasiwasi inayoshuhudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kuwa ni changamo kubwa kwa amani na usalama duniani.
-
Al Azhar yalaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina
Dec 01, 2022 04:01Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kwa mara nyingine tena kimeutaka ulimwengu uzingatie machungu na mateso ya taifa la Palestina na kukaliwa kwa mabavu ardhi sambamba na kulaani jinai za umwagaji damu zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi Wapalestina.
-
Theluthi moja ya wanajeshi wa kike wa Israel wamebakwa na makamanda wao
Dec 01, 2022 00:31Imeelezwa kuwa mmomonyoko wa kimaadili unazidi kukithiri katika jeshi na vyombo vingine vya usalama huko Israel huku kukiripotiwa kila uchao vitendo vya kubakwa na kunajisiwa wanajeshi na polisi wa kike.
-
Bunge la Kuwait lapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel
Dec 01, 2022 00:31Wabunge wa Kuwait wamepinga vikali hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Kanali ya Kizayuni: Israel inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina
Nov 30, 2022 07:15Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimesema hali ya usalama katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu ni ya 'hatari' na kwamba Tel Aviv inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina.
-
Wazayuni wameshaua shahidi Wapalestina 205 tangu mwanzoni mwa 2022
Nov 30, 2022 03:06Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti yake na kusema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshaua shahidi Wapalestina 205 katika sehemu mbalimbali za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
-
Ripoti kuhusu jinai za kivita za muungano wa Saudia na Imarati nchini Yemen
Nov 30, 2022 02:21Kituo cha sheria cha Ain al-Insaniyah (Jicho la Ubinadamu) cha Yemen kimetoa takwimu za kushtua kuhusu maafa ya kibinadamu na kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mashambulio ya muungano vamizi wa Saudia na Imarati katika nchi hiyo, takwimu ambazo zinaanika wazi wigo wa jinai za kivita zilizofanywa na muungano huo na waungaji mkono wake wa Magharibi na Wazayuni.