-
Hamas yamkosoa Waziri Mkuu wa Uingereza aliyesema yeye ni "Mzayuni mkubwa"
Oct 05, 2022 09:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imemkosoa Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss kwa kujiita "Mzayuni mkubwa" anayetaka kuimarisha uhusiano wa London na Tel Aviv, ikisema matamshi hayo yanalingana na Azimio la Balfour la Uingereza la 1917, ambalo liliweka msingi wa kuundwa utawala bandia wa Israel na kukoloniwa Palestina.
-
Hamas: Kucheza muziki ndani ya Msikiti wa Nabii Ibrahim ni uchochezi dhidi ya Waislamu
Oct 04, 2022 23:32Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa, sherehe ya kucheza ngoma na muziki ya walowezi wa Kizayuni ndani ya Msikiti wa Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron) ni jinai ya Kizayuni na kitendo hatari kinachochochea moja kwa moja hisia za Waislamu.
-
Jumblatt na Netanyahu: Israel imesalimu amri kwa Hizbullah ya Lebanon
Oct 04, 2022 08:01Kiongozi wa Chama cha Maendeleo cha Kisoshalisti cha Wadruzi wa Lebanon amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel umesalimu amri kwa nguvu za Hizbullah katika kadhia ya uchoraji mipaka ya baharini.
-
Sheikh Isa Qassem: Utawala wa Aal Khalifa unataka kuwafanya Wabahrain watumwa
Oct 04, 2022 07:25Ayatullah Sheikh Isa Qassem, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Bahrain amesema, utawala wa kifalme wa Aal Khalifa unataka kuwafanya watu wa nchi hiyo watumwa.
-
Lebanon na Israel zakaribia kufikia makubaliano ya kuweka mipaka ya baharini
Oct 04, 2022 02:49Taarifa zinaonyesha kuwa rasimu ya mwisho iliyopokelewa kutoka upande wa Marekani kuhusu kuainisha mipaka ya bahari ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel itapelekea kupunguzwa tofauti kati ya pande hizo mbili.
-
Ujerumani yachochea vita dhidi ya Yemen kwa kuiuzia Saudia silaha
Oct 03, 2022 05:49Takriban wiki moja baada ya ziara ya Kansela wa Ujerumani Olaf Schultz nchini Saudi Arabia, Berlin kwa mara nyingine tena imeanza kuiuzia Saudia Arabia silaha na zana za kivita.
-
Utawala wa Kizayuni watiwa hofu na oparesheni za muqawama Ukingo wa Magharibi
Oct 02, 2022 22:56Kupamba moto na kupanuka Intifadha ya wananchi na mapigano ya silaha ya wanamapambano wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kumeulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhamishia zana zake nzito za kijeshi kaskazini mwa eneo hilo.
-
Matokeo ya kustaajabisha ya uchaguzi wa Bunge la Kuwait, wafungwa watoka jela waingia Bungeni
Oct 02, 2022 04:43Matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Kuwait yamewashangaza wengi. Wapinzani wamepata viti vingi, nafasi ya Waislamu wa madhehebu ya Kishia nayo imeimarika kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea na wafungwa wawili wametoka jela na kuingia bungeni.
-
Nasrullah: Iran ni thabiti, haitatikiswa na matukio ya sasa
Oct 01, 2022 23:40Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ina nguvu na uthabiti kuliko wakati wowote ule, na kwamba taifa hili litavuka salama mtihani wa sasa kutokana na hekima ya viongozi wake.
-
Sanad yalaani kuongezeka hukumu za kikatili nchini Saudi Arabia
Oct 01, 2022 22:44Shirika la kutetea haki za binadamu la "Sanad" limetangaza kuwa kumeshuhudiwa ongezeko la kukamatwa wakosoaji na hukumu za kikatili na kidhalimu nchini Saudi Arabia katika kipindi cha hivi karibuni.