-
HAMAS: Muqawama una uungaji mkono mkubwa wa Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi
Aug 17, 2022 02:37Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiisalamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama uko chini ya mwavuli wa uungaji mkono wa kivitendo wa Wapalestina na jambo hilo ndilo linalozidi kutia nguvu harakati za muqawama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Wapalestina wafichua njama ya Israel ya kuubomoa kikamilifu msikiti wa Al Aqsa
Aug 16, 2022 22:10Duru za Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu zimefichua njama ya awamu tatu iliyoandaliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwa lengo la kuubomoa msikiti mtukufu wa Al Aqsa.
-
Iraq katika mkondo wa kushtadi zaidi mkwamo wa kisiasa
Aug 16, 2022 22:04Uamuzi wa makundi na mirengo ya kisiasa ya Iraq wa kufanya mikusanyiko ya barabarani umeifanya anga ya kisiasa ya nchi hiyo kuwa tete zaidi na mkwamo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo kushtadi zaidi.
-
Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza
Aug 16, 2022 09:34Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwaua watoto watano Wapalestina katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku
Aug 16, 2022 03:09Marekani inapora asilimia 80 ya mafuta yanayozalishwa kwa siku nchini Syria.
-
HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina
Aug 15, 2022 22:12Mjumbe mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama na mapambano ndio njia bora kabisa ya kuzikomboa ardhi za Palestina na kuifanya Palestina kuwa huru.
-
Karzai: Wananchi wa Afghanistan wametaabika mno kwa kuweko majeshi ya Marekani nchini kwao
Aug 15, 2022 22:11Hamid Karzai Rais wa zamani wa Afghanistan amesema kuwa, wananchi wa nchi hiyo wamedhurika pakubwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita ya kuweko majeshi ya kigeni yakiwemo ya Marekani katika nchi yao.
-
DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi
Aug 15, 2022 06:07Mtaalamu mmoja wa masuala ya kiusalama amesema, asilimia 90 ya wahanga na waathirika wa ugaidi nchini Iraq hasa katika maeneo yaliyokombolewa wameuliwa kwa silaha za Marekani.
-
Balozi mpya wa Kuwait aaanza kufanya kazi nchini Iran baada ya miaka 7
Aug 15, 2022 05:47Badr Abdullah Al-Manikh, balozi mpya wa Kuwait katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumamosi, mwanzoni mwa kazi yake, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdullahian, na kumkabidhi nakala ya vitambulisho vyake.
-
Israel kuanzisha vituo vya Wazayuni waliochanganyikiwa kiakili kutokana na vita vya Ghaza
Aug 15, 2022 01:50Wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wametangaza mpango wa kuanzisha vituo maalumu vya kuwatibu akili Wazayuni kutokana na athari mbaya za makombora ya Ghaza yanayovurumishwa kwenye vitongojia vya walowezi wa Kizayuni kujibu jinai za Israel.