Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku
Marekani inapora asilimia 80 ya mafuta yanayozalishwa kwa siku nchini Syria.
Wizara ya Mafuta ya Syria imesema vikosi vamizi vya Marekani vinaiba mapipa 66,000 za mafuta ghafi kwa siku katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, kiwango hicho kinachoibiwa na wanajeshi vamizi wa Marekani katika nch hiyo inayoshuhudia vita tangu mwaka 2011, ni sawa na asilimia 83 ya mafuta yanayozalishwa kila siku nchini humo.
Kwa muda sasa, wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kupora mafuta ghafi ya petroli katika maeneo wanayoyakalia kwa mabavu nchini Syria.

Hivi karibuni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova alisema Marekani inachukua kinyume cha sheria mafuta ghafi ya petroli yenye thamani ya dola milioni 30 kwa mwezi kutoka visima vya mafuta vilivyoko kaskazini mashariki mwa Syria.
Jeshi la Marekani ambalo linashirikiana na makundi ya kigaidi kwa muda mrefu limeweka kambi kinyume cha sheria katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Syria. Mbali na kupora mafuta ghafi ya petroli na ngano, limekuwa pia likishambulia askari na watu wa Syria. Marekani ni muuungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi nchini Syria.