Israel yamuua kigaidi mtaalamu mwingine wa nyuklia wa Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i133254-israel_yamuua_kigaidi_mtaalamu_mwingine_wa_nyuklia_wa_misri
Ingawa maafisa wa Misri wametangaza kwamba wamemkamata mhusika wa mauaji ya mwanasayansi kijana wa nyuklia wa nchi hiyo; lakini taarifa nyingine zinasisitiza kwamba muuaji aliondoka eneo la tukio mbele ya macho ya kila mtu na inaaminika ana uhusiano na shirika la kijasusi la Israel MOSSAD hasa kwa kuzingatia kuwa, Tel Aviv ina historia chafu ya kufanya jinai kama hizo za kuwaua kigaidi wanasayansi wa nyuklia wa nchi mbalimbali ikiwemo Misri.
(last modified 2025-11-16T10:58:55+00:00 )
Nov 16, 2025 10:58 UTC
  • Israel yamuua kigaidi mtaalamu mwingine wa nyuklia wa Misri

Ingawa maafisa wa Misri wametangaza kwamba wamemkamata mhusika wa mauaji ya mwanasayansi kijana wa nyuklia wa nchi hiyo; lakini taarifa nyingine zinasisitiza kwamba muuaji aliondoka eneo la tukio mbele ya macho ya kila mtu na inaaminika ana uhusiano na shirika la kijasusi la Israel MOSSAD hasa kwa kuzingatia kuwa, Tel Aviv ina historia chafu ya kufanya jinai kama hizo za kuwaua kigaidi wanasayansi wa nyuklia wa nchi mbalimbali ikiwemo Misri.

Mhandisi kijana wa kemia ya nyuklia nchini Misri aliuliwa kigaidi Jumatano kwa kupigwa risasi na gaidi asiyejulikana. Alipigwa risasi 13 na gaidi huyo na baadaye kutoweka mbele ya macho ya kila mtu. 

Toleo la mtandaoni la Jarida la Rai al-Youm limechapisha makala iliyoandikwa na Khaled al-Jayousi na kuandika: Tukio hilo linaonekana wazi kuwa kuwa ni kazi ya shirika la kijasusi la Israel Mossad. Ingawa hakuna uthibitisho kutoka kwa wahusika rasmi; lakini aliyeuawa si mtu wa kawaida; bali ni mhandisi wa kemia ya nyuklia ambaye alikuwa kijana wa umri wa miaka 35 tu; hivyo inaonekana wazi kwamba mtaalamu huyo alikuwemo kwenye orodha ya wataalamu wa nyuklia waliokuwa wanasakwa na magaidi wa Israel ili wauliwe kigaidi.

Makala hiyo ya gazeti la Rai al-Youm imeendelea kusema: Mkemia huyo wa nyuklia raia kijana wa Misri alipigwa risasi 13 tena barabarani hiyo ikiwa na maana kwamba upande uliopanga ugaidi huo ulitoa amri mauaji yatekelezwe kikamilifu na kusiwe na chembe ya makosa.

Maafisa wa Misri wamesema kuwa operesheni hiyo haikuwa na msukumo wa kisiasa. Wananchi wa Misri wamesikitishwa mno na ugaidi huo. 

Sehemu nyingine ya makaala hiyo imesema kuwa maafisa wa Misri wanasisitiza kwamba mhusika wa jinai hiyo ni mgonjwa wa akili suala ambalo limezua maswali mengi yasiyo na majibu, kwa sababu ugaidi aliofanya unahitaji mtu mwenye akili sana kuweza kuupanga na kuutekeleza.