Qalibaf: Israel haijawahi kuonja moto kama wa Vita vya Siku 12
-
Mohammad Bagher Qalibaf
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kwamba: Israel ilikumbaa na mashinikizo makubwa ya kukabiliana na mashambulizi ya Iran hususan katika siku za mwisho za Vita vya Siku 12 na haijawahi kupata kipigo kama ilichopata wakati wa vita vya siku 12 ilivyovianzisha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa Pars Today, Mohammad Bagher Qalibaf amefafanua zaidi kwa kusema: Utawala mtenda jinai na donda la saratani, utawala pandikizi wa Israel haujawahi kuonja moto na nguvu kubwa dhidi yake katika maisha yake yote ya miaka 80 iliyojaa balaa na hatima mbaya, kama ilivyochezea kipigo kwenye Vita vya Siku 12 wakati ilipoivamia kijeshi Iran.
Amesema: Katika siku 4-5 za mwisho za vita vya siku 12, Israel ilikuwa chini ya mashinikizo makubwa kutokana na kushindwa kukabiliana na mashambulizi ya Iran na kwamba Wazayuni walitamani muda wote kusimamisha mapigano. Nguvu hiyo ya taifa la Iran imetokana na masomo waliyopata vijana wa Iran kutoka kwa mashahidi Tehrani-Moghadam, Hajizadeh, Bagheri, Salami, Rashid, Soleimani, Mehrabi, Rabbani, Shadmani, Hamedani, Shushtari, Kazemi na wengineo wengi.
Spika wa Bunge la Iran pia amsema: Shahidi Tehrani-Moghadam na watu kama yeye walikuwa wakifanya kazi kubwa ya jihadi. Kwa kweli walikuwa na ujasiri wa kimantiki na kiakili. Walifanya maamuzi ya kustaajabisha. Shahid Tehrani-Moghadam alikuwa akisema mara kwa mara kwamba ikiwa hatutofanya kazi leo, kesho tutakuwa tumechelewa.
Spika Qalibaf pia amesema, wenyewe tumeona katika vita vya siku 12 kwamba kama tusingekuwa tumejizatiti mapema na lau kama tusingekuwa na nguvu kubwa za makombora, ingekuwa tatizo kubwa kwetu.
Amesema: "Somo muhimu zaidi lililotolewa na Shahid Tehrani-Moghadam kuliko hata kuunda makombora lilikuwa ni kujenga moyo wa kujiamini taifa la Iran na katika jamii tena milele.