-
Watetezi wa haki za binadamu walaumu Israel kwa kuwaua wafungwa wa Kipalestina
Aug 14, 2022 21:57Kundi moja la kutetea haki za binadamu limeushutumu utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na unyanyasaji wake wa kinyama na hatua kali dhidi ya wafungwa wa Kipalestina, likisema kwamba wafungwa hao wanakabiliwa na aina mbalimbali za mateso katika vizuizi na wanapoteza maisha.
-
Marekani yashadidisha vitendo vyake vya ujasusi nchini Iraq
Aug 14, 2022 06:51Ndege za Marekani hivi sasa zimeanzisha operesheni nyingi za kijasusi ambazo hazijawahi kushuhudiwa tangu walipoivamia na kuikalia kwa mabavu Iraq mwaka 2003. Operesheni hizo zimejikita katika kambi ya kijeshi ya Ain al Assad kuelekea ndani ya ardhi ya nchi jirani ya Syria.
-
Magaidi 50 wa Daesh wahamishiwa Iraq kutoka nchini Syria
Aug 13, 2022 22:01Kitengo cha upashaji habari cha jeshi la Iraq kimetoa ripoti rasmi na kusema kuwa karibu wanachama 50 wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Dashe (ISIS) wamehamishiwa mkoani Nainawa (Nineveh) Iraq kutoka katika kambi ya al Hawl ya nchini Syria.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu kuinuliwa hadhi ya Harakati ya Jihad Islami
Aug 13, 2022 04:06Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, "mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hiyo katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo."
-
HAMAS yapongeza misimamo ya waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya Israel
Aug 13, 2022 03:48Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amepongeza msimamo thabiti ulioonyeshwa na waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Mapigano kati ya mamluki wa Saudia na UAE kusini mwa Yemen; kuendelea mzozo wa kijiografia na kisiasa
Aug 12, 2022 21:00Wanamgambo wenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia wamepigana tena katika maeneo ya kusini mwa Yemen, hali ambayo imesababisha vifo na majeruhi kadhaa.
-
Wanamichezo Wairaq wakataa kupambana na timu ya Israel katika mashindano ya Romania
Aug 12, 2022 08:03Wanamichezo wawili Wairaqi wa mchezo wa tenisi wamekataa kupambana na wanamichezo kutoka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika michuano ya Paralampiki inayofanyika nchini Romania.
-
Israel imewaua shahidi watoto Wapalestina zaidi ya 1,000 tangu 2008
Aug 12, 2022 03:10Tangu mwaka 2008, zaidi ya watoto elfu moja wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel
-
Athari za mashambulio ya Yemen zinaendelea, Wakuwait wakatazwa kutumia drone Imarati
Aug 11, 2022 21:54Athari za mashambulio ya kulipiza kisasi na ya kujihami ya wananchi wa Yemen dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) bado zingalipo na sasa serikali ya Kuwait imewataka wananchi wake wasitumie ndege yoyote isiyo na rubani wanapokuwa nchini Imarati, ili wasije wakajiingiza kwenye matatizo.
-
Oman haitafuata nyayo za Saudia za kuruhusu ndege za Israel zitumie anga yake
Aug 11, 2022 06:35Oman imeripotiwa kukataa kuruhusu ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake, ikionekana kujiepusha kufuata nyayo za Saudi Arabia za kujikurubisha wazi wazi na utawala huo haramu.