-
Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon
Jul 31, 2022 07:04Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini.
-
Makumi ya viongozi wa serikali ya Saudia watiwa mbaroni kwa kula rushwa
Jul 31, 2022 02:55Serikali ya Saudi Arabia imewatia mbaroni maafisa 78 wa serikali kwa tuhuma za ufisadi, kula rushwa, utapeli, kutakatisha fedha na kutumia vibaya madaraka yao.
-
UN: Jela za siri za Imarati nchini Yemen zinatumiwa kutesa mahabusu
Jul 30, 2022 23:06Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ghasia na mateso katika jela za siri za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) huko Yemen.
-
Wafuasi wa mrengo wa Sadr wavamia tena jengo la Bunge la Iraq
Jul 30, 2022 23:01Wafuasi wa mrengo wa Sadr wamevamia tena kwa mara ya pili jengo la bunge la Iraq zikiwa zimepita chini ya siku tatu tangu walipovamia jengo hilo lililoko kwenye eneo lenye ulinzi mkali katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad.
-
Mgogoro Iraq; Bunge lavamiwa huku nara zikipigwa dhidi ya Waziri Mkuu aliyependekezwa
Jul 30, 2022 23:01Mamia ya wananchi wa Iraq tarehe 27 mwezi huu wa Julai waliandamana katika Eneo la Kijani katika mji mkuu Baghdad na kisha wakavamia Bunge na kupiga nara na shaari dhidi ya mwanasiasa aliyependekezwa kwa ajili ya nafasi ya Waziri Mkuu.
-
Macron akosolewa kwa 'kumtandikia zulia jekundu muuaji wa Khashoggi'
Jul 29, 2022 23:16Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wamemkosoa vikali Rais Emmanuel Macron wa Ufarasa kwa kumpokea Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ambaye anatuhumiwa kutoa amri ya kuuawa mwanahabari Jamal Khashoggi, huko nchini Uturuki miaka 4 iliyopita.
-
Kuwasilisha mashtaka Iraq dhidi ya Uturuki UN na kuongezeka hisia za chuki dhidi ya Ankara ndani ya Iraq
Jul 29, 2022 23:10Baada ya Iraq kuwasilisha mashtaka rasmi Umoja wa Mataifa dhidi ya Uturuki, Baraza la Usalama la umoja huo limeitisha kikao cha dharura, ambapo mbali na kulaani shambulio la mizinga lililolenga mkoa wa Duhok, limetangaza uungaji mkono wake pia kwa umoja wa ardhi yote, uhuru na mamlaka ya kujitawala ya Iraq.
-
Makundi ya mapambano ya Palestina yapinga tuhuma za Wazayuni wa Israel
Jul 28, 2022 21:57Makundi ya wanamapambano wa Palestina yamejibu tuhuma zilizotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel uliodai kufichwa silaha za wapigania uhuru katika makazi ya raia huko Gaza.
-
Nukta nne za kistratijia katika matamshi ya Sayyid Nasrullah kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 40 ya Hizbullah
Jul 27, 2022 07:44Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, juzi usiku (tarehe 25 Julai) alizungumza na televisheni ya al-Mayadeen kwa mnasaba wa mwaka wa 40 wa kuasisiwa Hizbullah, ambapo nukta kadhaa za kistratijia zilijadiliwa.
-
Sana'a: Mzingiro dhidi ya Yemen unazuia kurefushwa muda wa usitishaji vita
Jul 27, 2022 07:20Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Sana'a amelaani kuzingirwa wananchi wa Yemen na kuitaja hatua hiyo kuwa inazuia kurefushwa muda wa usitishaji vita nchini humo.