-
Amir wa Qatar amshukuru Rais wa Iran kwa mapokezi mazuri
May 13, 2022 03:15Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter ambapo amemshukuru Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mapokezi mazuri na ukarimu wakati wa ziara yake mjini Tehran.
-
Mabunge ya Kiislamu yatakiwa yatambue kuwa ni uhalifu kuanzisha uhusiano na Israel
May 12, 2022 21:55Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeyataka Mabunge ya Kiislamu kulitambua suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kuwa ni kosa na uhalifu.
-
Amir-Abdollahian: Wananchi wa asia Magharibi wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel
May 12, 2022 21:55Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa eneo la Asia Magharibi hawakubaliani na suala la kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya Wapalestina.
-
UN yaishukuru Iran kwa msaada wake katika jitihada za kutatua mzozo wa Yemen
May 12, 2022 21:52Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen amesifu na kupongeza msaada wa Iran kwa shirika hilo katika jitihada za kutatua mgogoro wa Yemen.
-
Dola milioni 79 zinahitajika kunusuru meli iliyo hatarini kuzama Yemen
May 12, 2022 06:53Takribani dola milioni 38 zimechangishwa kati ya 79.6 zinazohitajika ili kunusuru meli ya kuhifadhi mafuta, FSO Safer iliyo hatarini kuzama na kuvujisha mafuta au kulipuka kando mwa pwani ya Yemen katika Bahari ya Sham.
-
Haaretz: Jeshi la Israel limekiri kumuuwa Shireen Abu Akleh
May 12, 2022 03:29Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni baada ya kufanyika uchunguzi kuhusu kuuliwa ripota wa televisheni ya al Jazeera katika mji wa Jenin limekiri kuwa mwandishi huyo wa habari ameuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo.
-
Kuwaua kigaidi waandishi wa habari, mbinu chafu ya Wazayuni ya kujaribu kuficha jinai zake
May 12, 2022 02:49Mapema jana Jumatano, mwandishi wa habari ya televisheni ya al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi na kuuliwa shahidi kwa damu baridi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.
-
Balozi wa Palestina UN: Utawala wa Kizayuni ndio unaohusika na mauaji ya Shahidi Abu Akleh
May 11, 2022 22:42Balozi wa Palestina Umoja wa Mataifa amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio unaohusika na mauaji ya Shahidi Shireen Abu Akleh na akasisitiza kwamba, hawaukubali uchunguzi utakaofanywa na "maafisa wa utawala ghasibu wa Israel" kuhusu mauaji hayo.
-
Sababu ya Israel kuuchukulia kuwa 'malaika wa uokozi' uuzaji silaha na kuanzisha uhusiano wa kawaida na nchi ndogo za Kiarabu
May 11, 2022 21:54Kila utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unapohisi unakabiliwa na mbinyo mkali wa ndani na katika eneo, hususan pale unaposhindwa kujidhaminia usalama wake, huliibua haraka suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya nchi za Kiarabu, ili kwa njia hiyo uweze kujitoa kwenye mashinikizo na kutaka uonekane pia kwamba hauko peke yake, bali kuna nchi kadhaa ambazo ziko pamoja nao.
-
Umoja wa Mataifa: Mamilioni ya Wasyria wanahitaji msaada wa kibinadamu ndani na nje ya nchi
May 11, 2022 21:50Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa, mgogoro wa Syria unaendelea kuwa changamoto kila uchao kwa wananchi na serikali ya nchi hiyo.