-
Oman yataka ukombozi wa Palestina na kukomeshwa kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni
Apr 27, 2022 22:17Nchi ya Oman imetaka jamii ya kimataifa itekeleze majukumu yake ya kukomesha kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni ardhi za Palestina kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.
-
Muqawama wa kutumia silaha; aina bora kabisa ya kupambana na utawala wa Kizayuni
Apr 27, 2022 22:12Makundi ya muqawama ya Palestina yametoa tamko la pamoja katika wakati huu wa kukaribia mno Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni kesho Ijumaa tarehe 29 Aprili 2022 na mbali na kuashiria jinai za utawala wa Kizayuni yamesema kwamba, mapambano ya kutumia silaha ndio muqawama bora kabisa wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni.
-
Khatibu wa Masjidul Aqswa: Kuanzisha uhusiano na Israel hakutakuwa na taathira kwa muqawama wa Palestina
Apr 27, 2022 03:35Khatibu wa Masjidul Aqswa amesema kuwa, kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel kulikofanywa na baadhi ya mataifa ya Kiarabu hakutakuwa na taathira yoyote kwa muqawama na mapambano ya taifa la Palestina.
-
Ismail Hania: Kadhia ya Quds haiwezi kupatiwa ufumbuzi kupitia njia ya mazungumzo
Apr 27, 2022 03:34Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, wimbi jipya la muqawama ni sisitizo kwamba, kadhia ya Quds, msikiti wa al-Aqswa, haki ya kurejea wakimbizi na kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina ni mambo ambayo hayawezi kupatiwa ufumbuzi kwa kukukaa katika meza ya mazungumzo.
-
Siku ya Kimataifa ya Quds ni dhihirisho la umoja wa Umma wa Kiislamu
Apr 26, 2022 23:16Msemaji wa Idara ya Mahakama ya Iran ameashiria kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds na kuitaja siku hiyo kuwa dhihirisho la umoja wa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuukomboa mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem).
-
Barghouti: Israel imeshindwa na wanamapambano wa Palestina
Apr 26, 2022 06:23Mwanasiasa wa ngazi za juu wa Palestina anasema miradi ya utawala haramu wa Israel imeporomoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwani utawala huo ghasibu umeshindwa kukabiliana na muqawama wa Palestina.
-
OIC: Mji wa Quds na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Umma wa Kiislamu
Apr 26, 2022 03:14Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuwa, mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas pamoja na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Umma wa Kiislamu na amani na utulivu hauwezi kupatikana bila ya kukombolewa maeneo hayo matakatifu kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni.
-
Wasiwasi na matumaini ya duru ya tano ya mazungumzo ya Iran na Saudi Arabia
Apr 25, 2022 23:18Kufanyika duru ya tano ya mazungumzo kati ya Iran na Saudi Arabia huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq, kumetoa matumaini ya kufanyika duru ya sita ya mazungumzo hayo.
-
Sana'a: Umoja wa Mataifa ni mshirika wa mzingiro dhidi ya Yemen
Apr 25, 2022 22:40Maafisa wa Yemen wameuonyeshea tena kidole cha lawama Umoja wa Mataifa na kuitaja asasi hiyo ya kimataifa kuwa mshirika wa mzingiro dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
-
Nasrullah atahadharisha kuhusu njama za kuitumbukiza Lebanon katika mzozo baada ya ajali ya boti
Apr 25, 2022 06:21Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah ametahadharisha juu ya njama zenye lengo la kuibua machafuko katika nchi hiyo ambayo imeathiriwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Sayyid Hassan Nasrullah ameeleza haya baada ya boti kuzama mashariki mwa bahari ya Mediterania.