-
Imarati yaomba msaada wa haraka kwa Wazayuni baada ya kipigo cha operesheni "Kimbunga cha Yemen"
Jan 20, 2022 23:47Imarati imeukimbilia utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuomba msaada wa haraka baada ya operesheni kubwa ya shambulio "Kimbunga cha Yemen" iliyolenga mji wa Abu Dhabi na kusababisha hasara kubwa kwa nchi hiyo ya mali na roho za watu.
-
Nchi nne za Ulaya zataka kusimamishwa ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu
Jan 20, 2022 07:07Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi nne za Ulaya ambazo ni Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania wamesema kuwa uamuzi wa viongozi wa utawala haramu wa Israel wa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Safari tarajiwa ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Uturuki
Jan 20, 2022 06:05Baadhi ya matukio ya miaka ya hivi karibuni yanaonyesha kuwepo mkakati maalumu wa kuanzishwa tena uhusiano wa karibu baina ya Uturuki na utawala wa kibaguzi wa Israel.
-
HAMAS: Taifa la Palestina ndilo litakalopata ushindi wa mwisho mbele ya Israel
Jan 20, 2022 04:41Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, taifa la Palestina ndilo litakalopata ushindi wa mwisho mbele ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Utawala ghasibu wa Kizayuni washadidisha kamatamata dhidi ya raia wa Palestina
Jan 19, 2022 06:53Wazayuni maghasibu wamebomoa nyumba kadhaa za raia wa Palestina na kuwatia mbaroni Wapalestina 27 ikiwa ni katika kuendelea uadui na chuki za utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wakazi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Saudia yaua raia wa Yemen, ikiwemo familia nzima, katika hujuma dhidi ya Sana'a
Jan 18, 2022 23:32Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesema muungano wa kivita wa Saudi Arabia umetekeleza mashambulizi dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a, ambapo raia 20, ikiwemo familia moja wameuawa.
-
Yemen: Kama Imarati itaendelea kuua watu wetu, tutasambaratisha uchumi wake
Jan 18, 2022 09:58Kamanda Mkuu wa majeshi ya Yemen ameionya vikali nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na kusisitiza kuwa, kama Abu Dhabi itaendelea kushiriki katika mashambulizi na jinai dhidi ya wananchi wa Yemen, basi wanamapambano wa Yemen watasambaratisha uchumi wa UAE unaotegemea uwekezaji wa kigeni.
-
Mashambulio ya Wayamen dhidi ya Imarati; malengo na umuhimu wake
Jan 18, 2022 07:39Jumatatu ya jana tarehe 17 Januari, ndege 20 zisizo na rubani pamoja na makombora 10 ya balestiki ya Jeshi na Kamati za Kujitolea za Wananchi wa Yemen zilishambulia maeneo muhimu na nyeti ndani ya ardhi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).
-
Undumakuwili wa Umoja wa Ulaya: Mapigano Yemen yanaweza kuhitimishwa kwa njia ya kisiasa tu
Jan 18, 2022 03:47Umoja wa Ulaya umetoa taarifa katika radiamali yake kwa mashambulizi ya kuadhibu ya jeshi la Yemen huko Abu Dhabi na kusisitiza kuwa mapigano yanayoendelea Yemen yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya kisiasa tu.
-
Muungano vamizi wa Saudia waushambulia mji mkuu wa Yemen, Sana'a
Jan 17, 2022 23:45Duru za habari jana usiku ziliripoti kuwa ndege za kivita za muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia zimefanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a.