-
Je, Muqawama wa Yemen Ulishindaje Mkakati wa Saudi Arabia?
Sep 14, 2026 09:27Kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini Yemen, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ikisisitiza kuwa kutatuliwa matatizo ya Yemen hakuwezekani kupitia kuendelezwa mzingiro na utunishaji misuli ya kijeshi.
-
Moto warindima katika Kitovu cha Usafirishaji Mafuta Saudi Arabia
Sep 14, 2026 07:35Vyombo mbalimbali vya habari jana Jumapili vilisambaza picha zinazoonesha moshi mzito ukifuka kutoka kwenye kituo cha mafuta vya Yanbu katika pwani ya Bahari ya Shamu. Taarifa zinasema kuwa, kituo hicho ndicho kilichokuwa kinaisaidia Marekani kupakia mafuta baada ya Iran kufunga Lango-Bahari la Hormuz.
-
Yemen yashambulia kambi ya kijeshi ya Saudia kwa makombora na ndege zisizo na rubani kulipiza kisasi
Sep 13, 2026 11:22Majeshi ya Jamhuri ya Yemen (YAF) yametekeleza operesheni kubwa ya pamoja ya makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudia katika eneo la Sharurah mkoani Najran kusini mwa ufalme huo, ikiwa ni jibu kwa kuendelea mashambulizi ya Saudia dhidi ya ardhi ya Yemen.
-
Mufti wa Oman: Umma wa Kiislamu umekumbwa na fitina kubwa
Sep 13, 2026 07:20Mufti wa Oman, Sheikh Ahmed Al-Khalili, amekosoa misimamo ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusu Ansarullah ya Yemen, akieleza kuwa, hali imekuwa ya hatari kutokana na kuzuka tena mapigano nchini humo.
-
Askari wa Israel asema waliambiwa: 'Mnao watu milioni mbili wa kuwalenga shabaha Ghaza'
Sep 13, 2026 07:05Askari wa akiba wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel amesema, maafisa wa jeshi hilo wanaichukulia idadi yote ya Wapalestina milioni mbili wa Ukanda wa Ghaza kama walengwa halali wa kuuawa, na amesimulia mauaji mengi yaliyofanywa na askari wa kizayuni na jinsi utekelezaji wa kanuani za vita ulivyoporomoka wakati wa mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa eneo hilo.
-
Uzalishaji wa mafuta wa Saudia umeshuka hadi kiwango cha chini zaidi cha tangu 1990; sababu ni vita vya US dhidi ya Iran
Sep 13, 2026 07:02Uzalishaji wa mafuta ghafi wa Saudi Arabia ulishuka hadi mapipa milioni 6.24 kwa siku mwezi Agosti, na kuashiria kiwango chake cha chini kabisa kilichoripotiwa tangu 1990, huku vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran vikiendelea kuvuruga mtiririko wa nishati katika Mashariki ya Kati.
-
Iran: Mamlaka ya kujitawala ya Yemen lazima yaheshimiwe, mzingiro haramu lazima ukomeshwe
Sep 12, 2026 04:31Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza tena msimamo wake thabiti na wa kimisngi kuhusu ulazima wa kuheshimiwa uhuru, mamlaka ya kitaifa ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Yemen, na kutoa wito wa kukomeshwa mara moja mzingiro haramu na usio wa kibinadamu uliowekwa dhidi ya nchi hiyo.
-
Axios: Trump amemkatalia Bin Salman ombi la kutaka Marekani iisaidie kijeshi Saudia dhidi ya Yemen
Sep 12, 2026 04:26Marekani imeyakataa maombi ya Saudi Arabia ya kuanzisha mashambulizi ya moja kwa moja ya kijeshi dhidi ya harakati ya Wahouthi ya Ansarullah nchini Yemen baada ya wapiganaji wa harakati hiyo kuuteka mji wa kimkakati wa pwani wa Mokha. Hayo ni kwa mujibu wa tovuti ya habari ya nchini Marekani ya Axios.
-
Jeshi la Yemen ladhibiti kikamilifu Lango Bahari Bab al-Mandab, pigo kubwa kwa wavamizi
Sep 11, 2026 09:26Jeshi la Yemen limefanikiwa kudhibiti kikamilifu Lango-Bahari muhimu mno la Bab al-Mandab baada ya kukikomboa kisiwa cha kimkakati cha Mayun. Hilo ni pigo kubwa kwa wavamizi wote wa Yemen.
-
Vikosi vya Yemen vyateka jiji la bandari la kimkakati la Bahari ya Sham la Mokha
Sep 11, 2026 04:14Vikosi vya Yemen Alhamisi vimedhibiti jiji la bandari la kimkakati la Bahari ya Sham la Mokha, huku vikielekea kwenye mlango-bahari muhimu wa Bab al-Mandab, hatua ambayo ni pigo kubwa kwa mamluki Saudi Arabia.