-
Uchaguzi wa Bunge la utawala wa Israel: Wapinzani wa Netanyahu wanaongoza katika kura za maoni
Sep 10, 2026 10:03Kura mpya ya maoni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel kuhusiana na uchaguzi wa bunge inaonyesha kuwa, wapinzani wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu bado wanaongoza.
-
Je, vita vimezidisha vipi hali ya kutengwa kielimu utawala wa Kizayuni?
Sep 10, 2026 05:50Tovuti ya Kizayuni ya Calcalist imeripoti kuwa sehemu ya Israel katika ufadhili wa utafiti wenye itibari wa Ulaya imepungua kwa kiasi kikubwa, huku kukiwa na ongezeko la visa vya watafiti wa kigeni wanaokataa kushirikiana na taasisi za Israel.
-
Ripoti: Watu 8,000 wamekatwa viungo tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza
Sep 10, 2026 03:19Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Quds (Qudsna), vyanzo vya Palestina vimeripoti kwamba tangu kuanza vita dhidi ya Gaza, visa 8,000 vya kukatwa viungo vya mwili vimeripotiwa. Aidha, katika hali ya sasa, watu 10,000 wenye ulemavu wa viungo wanahitaji huduma za urekebishaji na tiba ya viungo kwa dharura.
-
Mkuu wa zamani wa Shin Bet: Kwa sasa tunaelekea kushuhudia mwisho wa Israel
Sep 10, 2026 02:45Mkuu wa zamani wa Shirika la Usalama wa Ndani la Israel Shin Bet amesema kuwa, vita vinavyoanzishwa na Tel Aviv havina lengo la kisiasa, na kwamba Israel inaelekea katika mwisho wa mradi wa Kizayuni.
-
Ansarullah ya Yemen yaitaka Saudia ijiondoe kwenye gwanda na mwavuli wa Marekani na Israel
Sep 09, 2026 11:42Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeituhumu Saudi Arabia kuwa inatekeleza mipango ya Kizayuni katika eneo na kuwataka watawala wa Riyadh wajiondoe kwenye gwanda na mwavuli wa himaya ya Marekani na utawala wa Kizayuni.
-
Israel yaiamuru Uingereza ifunge ubalozi wake mdogo ulioko Baitul Muqaddas Mashariki
Sep 09, 2026 10:17Utawala wa kizayuni wa Israel umeutaarifu ubalozi mdogo wa Uingereza ulioko katika eneo la Baitul Muqaddas Mashariki (East Jerusalem) linalokaliwa kwa mabavu, kwamba lazima uwe umeshaufunga ubalozi huo ndani ya muda wa siku 30. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na kituo cha habari cha umma cha Israel KAN.
-
Baada ya kushtadi jinai za walowezi wa kizayuni, nchi 12 zatangaza marufuku ya biashara na vitongoji haramu
Sep 09, 2026 03:10Nchi 12 zimetoa taarifa ya pamoja zikitangaza marufuku ya kitaifa ya biashara kwa bidhaa zinazotoka kwenye vitongoji haramu vilivyojengwa na utawala wa kizayuni wa Israel katika maeneo ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi unayoyakalia kwa mabavu.
-
Yemen yaanzisha mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya vituo vya mafuta vya Aramco, Saudia Arabia
Sep 08, 2026 11:05Jeshi la Yemen limeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi inayolenga vituo vya mafuta vya Saudi Aramco na kambi za kijeshi za anga kusini mwa Saudi Arabia, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi cha moja kwa moja dhidi ya kampeni ya kikatili ya mashambulizi ya anga ya siku tatu iliyofanywa na Riyadh, ambayo ilijumuisha mauaji ya kutisha katika gereza moja nchini Yemen.
-
Vita vya kidini vya utawala wa Kizayuni: Marufuku ya kutoa adhana katika Msikiti wa Ibrahimi yaingia siku ya 75
Sep 07, 2026 11:41Katika kipindi cha siku 75 zilizopita, utawala wa Kizayuni, pamoja na kukiuka heshima ya Msikiti wa Ibrahimi katika mji wa Al-Khalil, umekiuka waziwazi uhuru wa kidini wa Waislamu kwa kuzuia kutolewa adhana katika eneo hilo takatifu la Kiislamu.
-
Nchi nane za Kiarabu na Kiislamu: Gaza ni eneo lisiloweza kutenganishwa na Palestina
Sep 07, 2026 03:05Nchi nane za Kiarabu na Kiislamu ambazo ni Saudi Arabia, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Pakistan, Uturuki, Qatar na Misri, zimetangaza kuwa, Ukanda wa Gaza ni sehemu isiyotenganishwa ya ardhi ya Palestina.