Pars Today
Hatua ya utawala wa Kizayuni ya kupiga marufuku shughuli za UNRWA imekabiliwa na radiamali kali za kimataifa.
Mamlaka za Palestina katika eneo la Beit Lahia kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza leo zimeutangaza mji huo kuwa "eneo la maafa" wakati jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linaendelea na mashambulizi yake ya kinyama na mauaji ya kimbari katika eneo hilo la Palestina.
Vyombo vya habari vya Kiebrania vimetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kufikia makubaliano na harakati ya Hamas yatakayowezesha kuachiliwa idadi ndogo ya mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Ghaza mkabala na kusitishwa mapigano kwa muda wa mwezi mmoja.
Zaidi ya waandishi elfu moja wameahidi kutoshirikiana na taasisi za kiutamaduni za utawala wa Kizayuni wa Israel, ambazo zinatajwa kushiriki katika ukiukaji wa haki za Wapalestina.
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Olmart amesema adui wa utawala huo sio Iran, Hizbullah wala Hamas bali ni Waisraeli wenye itiikadi kali akiwemo waziri mkuu wa sasa wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.
Wizara ya Elimu katika Ukanda wa Gaza imesema utawala wa Kizayuni wa Israel umewaua wanafunzi zaidi ya 11,852 katika eneo hilo lililozingirwa la Palestina, tangu Oktoba mwaka jana 2023.
Utawala wa Kizayuni ulioanzisha vita dhidi ya Lebanon kama ulivyotangaza kwamba ni kwa lengo kuwarejesha walowezi katika nyumba zao, hivi sasa unakabiliwa na ongezeko la walowezi wanaokimbia makazi yao, askari waliochoshwa na vita na majeruhi wengi.
Ndege za kivita za Israel zimeshambulia kwa mabomu jengo la makazi ya raia linalowahifadhi Wapalestina waliolazimika kuhama makazi yao kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuua makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi.
Sheikh Naim Qassim aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa harakati hiyo ya mapambano baada ya mtangulizi wake Sayyid Hassan Nasrullah kuuawa shahidi katika hujuma ya Israel kusini mwa Beirut, mwezi uliopita.
Takwimu rasmi za makadirio zilizochapishwa zinaonyesha kuwa, Marekani imetoa zaidi ya dola bilioni 22 za silaha na misaada ya kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita.