-
Al Qaeda yaungama hadharani kuwa inapigana bega kwa bega na Muungano wa Saudia Yemen
Jul 11, 2021 08:54Mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda umetoa taarifa ukikiri kwamba, katika vita vinavyoendelea katikati ya Yemen unapigana bega kwa bega na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya vikosi vya jeshi la Yemen na vile vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo.
-
Harakati ya Fat'h Palestina yataka UAE ifukuzwe katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Jul 11, 2021 08:50Mjumbe wa kamati kuu ya harakati ya Fat'h ya Palestina ametaka Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati ufukuzwe katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kuwapatia uraia raia wa utawala huo.
-
Hizbullah: Marekani itashindwa katika vita ya kiuchumi kama ilivyoshindwa katika vita vya kijeshi
Jul 11, 2021 03:38Mjumbe wa Kamati Kuu ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mhimili wa Marekani kama ulivyoshindwa katika vita vya kijeshi katika eneo la Asia Magharibi utashindwa pia katika vita vya kiuchumi.
-
Mahmoud Abbas ataka kung'olewa mizizi ya uvamizi wa Israel katika ardhi za Palestina
Jul 11, 2021 03:35Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza juu ya udharura wa kufanyika kazi ya kisiasa kwa ajili ya kung'oa mizizi ya uvamizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Palestina.
-
Hamas yawataka wakazi wa Ukingo wa Magharibi kudumisha mapambano dhidi ya Wazayuni
Jul 11, 2021 00:12Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imewataka wakazi wa Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan kudumisha mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuhakikisha kwamba ardhi ya Palestina inakuwa kaa la moto kwa maghasibu hao.
-
Harakati ya Hashdu Shaabi ingali na taathira kubwa katika mapambano dhidi ya magaidi
Jul 11, 2021 00:11Qassim Muslih Kamanda wa Oparesheni wa Harakati ya Hashdu Shaabi katika mkoa wa al Anbar huko Iraq hivi karibuni alifungwa jela kwa tuhuma zisizo na msingi kutokana na njama za baadhi ya pande na mirengo ya Iraq inayoungwa mkono na nchi ajinabi na yenye mfungamano na vyombo vya habari vya Saudia na Imarati katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Askari wa Kizayuni wawafyatulia risasi na kuwajeruhi mamia ya Wapalestina
Jul 10, 2021 07:48Askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamewafyatulia risasi na kuwajeruhi mamia ya Wapalestina waliokuwa wakiandamana kulalamikia ujenzi haramu wa kituo cha jeshi hilo ghasibu katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman: Katu hatutafanya mapatano na Israel
Jul 10, 2021 06:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono haki za kisheria za Palestina na katu haitafanya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kikao cha Tehran na mustakbali wa Afghanistan
Jul 10, 2021 05:42Kikao cha makundi ya Kiafghani ambacho kimefanyika hapa Tehran siku za Jumatano na Alhamisi kikihudhuriwa na wawakilishi wa serikali ya Afghanistan, shakhsia na ujumbe wa kisiasa wa ngazi ya juu wa kundi la Taliban chini ya uwenyeji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kilimaliza shughuli zake kwa kutolewa taarifa yenye vipengee sita.
-
Umoja wa Mataifa waitaka Israel iache kubomoa nyumba za Wapalestina
Jul 10, 2021 03:09Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala ghasibu wa Israel usitishe hatua zake za kubomoa nyumba na makazi ya wananchi wa Palestina