-
Misri yauonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Ukanda wa Ghaza
May 31, 2021 02:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, usiku wa kuamkia leo ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu hatari za kuvunja makubaliano ya kusimamisha vita ya Ghaza.
-
Sultan wa Oman naye ampongeza Bashar al Assad kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Syria
May 30, 2021 22:20Sultan wa Oman amemtumia ujumbe Rais Bashar al Assad wa Syria na kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.
-
Bunge Iraq kumsaili Waziri Mkuu juu ya uwepo wa askari wa Marekani nchini humo
May 30, 2021 08:54Mbunge mmoja wa Iraq ametangaza kuwa, bunge hilo litamwita na kumsaili Waziri Mkuu na baraza lake la mawaziri kuhusiana na yanayojiri nchini himo ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Iraq.
-
Sababu za kukasirishwa Netanyahu na azimio la Baraza la Haki za Binadamu la UN
May 30, 2021 06:30Viongozi wa utawala kandamizi na katili wa Kizayuni wamehamakishwa mno na hatua ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kupasisha muswada wa kuundwa kamati ya kuchunguza jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Bashar al Jaafari: Ushindi wa Syria ni ushindi dhidi ya njama za kigaidi
May 30, 2021 03:26Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa uchaguzi wa rais wa hivi karibuni nchini humo ulikuwa kielelezo cha ushindi wa taifa la Syria na kushindwa baadhi ya pande na kwamba Damascus imerejea katika diplomasia ya Kiarabu.
-
Makumi ya wanajeshi wa Saudia waangamizwa mkoa wa Jizan
May 30, 2021 03:16Operesheni iliyofanywa na jeshi la Yemen huko kusini mwa Saudi Arabia imeangamiza na kujeruhi makumi ya wanajeshi wa utawala huo wa kifalme.
-
Sababu za mivutano ya mara kwa mara katika uhusiano wa serikali ya Iraq na Hashdu Shaabi
May 29, 2021 23:24Katika siku za karibuni uhusiano wa serikali ya Mustafa al Kadhimi Waziri Mkuu wa Iraq na wapiganaji wa kundi la Hashdu Shaabi kwa mara nyingine tena umegubikwa na hali ya mivutano. Hali hiyo imejitokeza baada ya askari maalumu waliochini ya usimamizi wa Waziri Mkuu wa Iraq kumtia mbaroni Qassim Mosleh mmoja kati ya makamanda wa ngazi ya juu wa Hashdu Shaabi.
-
Balozi wa Palestina nchini Iran: Vita vya siku 12 vimefungua mlango wa kuangamizwa kikamilifu Israel
May 29, 2021 22:16Balozi wa Palestina nchini Iran amesema kuwa, vita vya siku 12 vilivyomalizika hivi karibuni baina ya utawala wa Kizayuni na wanamapambano wa Palestina, vimefungua mlango wa kuangamizwa kikamilifu Israel.
-
Mahmoud Abbas ampongeza Rais Bashar al Assad kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Syria
May 29, 2021 22:15Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemtumia ujumbe wa maandishi Rais Bashar al Assad na kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Syria.
-
Maafisa usalama wa Misri wawasili katika Ukanda wa Ghaza, Palestina
May 29, 2021 05:10Duru za habari zimetangaza kuwa ujumbe maalumu wa maafisa usalama wa Misri umewasili katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wakuu wa makundi ya muqawama.