-
Sheikh Naim Qassim: Hali ya kiafya ya Sayyid Hassan Nasrullah ni nzuri
May 28, 2021 22:28Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema hali jumla ya kiafya ya kiongozi wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah ni nzuri.
-
Hadi al-A'miri: Kudhoofisha nguvu za Hashd al Shaabi ni kudhoofisha nguvu za serikali ya Iraq
May 28, 2021 22:14Mwenyekiti wa Muungano wa Fat'h nchini Iraq amesema Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq, maarufu kama Hashd al Shaabi, kwa damu yake toharifu limeweza kuipa nguvu serikali ya Iraq na hivyo kila anayetaka kusambaratisha nguvu na uwezo wa jeshi hilo kimsingi atakuwa amedhoofisha nguvu za taifa la Iraq.
-
Wananchi wa Syria wafurahia ushindi wa Bashar al Assad, Wamagharibi wahamaki
May 28, 2021 02:25Baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini Syria ambapo Rais Bashar al Assad kwa mara nyingine ameshinda katika uchaguzi huo, wananchi wa maeneo mbalimbali ya Syria wamemiminika mitaani kusherehekea ushindi.
-
Leo Wapalestina wanafanya maandamano makubwa ya kupinga Uzayuni
May 27, 2021 22:11Vijana wa Palestina wametangaza kuwa, leo Ijumaa watafanya maandamano makubwa katika kona zote za Palestina, maandamano ambayo yatapewa jina la "Mapambazuko."
-
Udharura wa kushtakiwa wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa jinai zao za kivita
May 27, 2021 21:58Ukatili wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza ni mfano wa wazi wa mauaji ya kimbari, jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na ukiukwaji wa misingi ya kibinadamu. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, waliohusika na maovu hayo wanapaswa kukamatwa na kufikishwa katika mahakama za kimataifa.
-
Syria: Nchi za Magharibi uchaguzi wetu haukuhusuni ndewe wala sikio
May 27, 2021 06:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, nchi za Magharibi hazipaswi kujipa uthubutu wa kuzungumzia uchaguzi wa nchi hiyo kwani hauzihusu kwa mbali wala kwa karibu nchi hizo za kibeberu.
-
Nukta sita kuhusu uchaguzi wa rais nchini Syria
May 27, 2021 06:35Uchaguzi wa pili wa rais katika muongo mmoja uliopita nchini Syria ulifanyika jana Mei 26. Tunaweza kuashiria nukta kadhaa hapa kuhusu uchaguzi huo.
-
Baada ya kudhalilishwa Gaza, Israel sasa yaitishia vita Lebanon
May 27, 2021 03:20Baada ya kudhalilishwa na kushindwa vibaya na kambi ya muqawama katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, utawala wa Kizayuni wa Israel sasa unatishia kuishambulia kijeshi Lebanon.
-
HAMAS: Tuna uwezo wa kuvurumisha mamia ya makombora kwa dakika
May 27, 2021 03:00Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika Ukanda wa Gaza amesema harakati hiyo ya muqawama inayo uwezo wa kuvurumisha mamia ya makombora ndani ya dakika moja, yanayoweza kupiga umbali wa hadi kilomita 200, ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Malengo ya safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu
May 26, 2021 21:47Ikiwa ni siku nne tu zimepita tokea utawala haramu wa Israel ulazimike kusitisha hujuma yake ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza, Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amewasili Israel ambapo ameonana na kufanya mazungumzo na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo na kisha kuelekea Ramallah ambapo amekutana na kuzungumza pia na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kabla ya kuelekea Misri na Jordan kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.