Makumi ya wanajeshi wa Saudia waangamizwa mkoa wa Jizan
(last modified Sun, 30 May 2021 07:46:28 GMT )
May 30, 2021 07:46 UTC
  • Maiti za wanajeshi wa Saudia
    Maiti za wanajeshi wa Saudia

Operesheni iliyofanywa na jeshi la Yemen huko kusini mwa Saudi Arabia imeangamiza na kujeruhi makumi ya wanajeshi wa utawala huo wa kifalme.

Afisa mmoja wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa, operesheni hiyo kubwa ya jeshi imelenga maeneo ya jeshi la Saudi Arabia katika miinuko ya MBC, al Fukhaidha na al Bidha.

Afisa huyo anasema wapiganaji wa Yemen wanadhibiti kikamilifu maeneo hayo na wamesababisha hasara kubwa kwa askari wa adui. 

Awali maeneo hayo yalikuwa na kambi za wanajeshi wa Saudia, mamluki kutoka Sudan na wapiganaji wa kundi linalojulikana kwa jina la al Maghawir. 

Wapiganaji wa kujitolea wa Yemen

Habari zinasema idadi kadhaa ya maafisa wa jeshi la Saudi Arabia wameuawa katika operesheni hiyo na makumi ya wanajeshi wa nchi hiyo na mamluki kutoka Sudan wamekamatwa mateka. 

Saudi Arabia, ikiungwa mkono na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Machi 25 mwaka 2015 ilianzisha hujuma na mashambulizi makubwa huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu.  

Tags