-
Jihad Islami: Hatima ya wanajeshi wa Israel itakuwa ni kuuawa au kutekwa wakivamia Ghaza
May 14, 2021 03:50Harakati ya kupigania ukombozi wa Palestina ya Jihad Islami imesema endapo utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo utaanzisha vita vya nchi kavu dhidi ya Ghaza basi askari Wazayuni hawatakuwa na hatima nyingine ghairi ya kuuawa au kutekwa nyara na hivyo hiyo itakuwa njia rahisi zaidi kwa harakati za kupigania ukombozi au muqawama kupata ushindi.
-
Israel yaendeleza hujuma Ghaza, Wapalestina 109 wameuawa shahidi
May 14, 2021 01:22Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza hujuma ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Ghaza Alhamisi usiku ikiwa ni muendelezo wa jinai zake dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika eneo hilo. Wapalestina zaidi ya 109 wanaripotiowa kuuawa shahidi katika uvamizi wa Israel dhidi ya Ghaza katika kipindi cha siku chache zilizopita. Taarifa zinasema askari wa Kizayuni sasa wanatekeleza uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Ghaza
-
Safari ya Zarif mjini Damascus; uungaji mkono wa Iran kwa uchaguzi wa Syria
May 13, 2021 23:01Muhammad Jawad Zarif Waiziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonana na kuzungumza mjini Damascus na Rais Bashar Asad wa Syria kuhusu uhusiano wa pande mbili, matukio ya Asia Magharibi na uchaguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo.
-
Muhammad Ali al-Houthi azitaka Saudia na Imarati kusitisha vita Yemen na kwenda al-Aqswa
May 13, 2021 23:00Muhammad Ali al-Houthi, mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen ameitaka Saudi Arabia, Imarati pamoja na washirika wao kusitisha vita huko Ma’arib Yemen na badala yake kuelekea huko Palestina kwa ajili ya kuikomboa Masjidul-Aqswa.
-
Wazayuni wakiri kipigo, wameshapata hasara ya dola milioni 160 kwa mashambulio ya muqawama
May 13, 2021 07:23Chama cha Wazalishaji Bidhaa cha utawala wa Kizayuni kimetangaza kuwa, tangu yalipoanza mashambulizi ya makombora wanamapambano wa Palestina siku chache zilizopita hadi hivi sasa, sekta ya uzalishaji bidhaa ya Israel imeshapata hasara ya dola miliioni 160.
-
Maelfu ya Wapalestina washiriki katika Sala ya Idul Fitr kwenye Msikiti wa al Aqsa
May 13, 2021 07:07Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr leo Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
-
Safari ya Amir wa Qatar Saudi Arabia
May 13, 2021 04:19Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, tarehe 10 Mei alifanya safari chini Saudia Arabia ambapo alikutana na kuzungumza na Muhammad bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo.
-
Yemen yajibu mapigo, yashambulia kampuni ya mafuta ya Aramco na uwanja wa ndege wa Najran, Saudia
May 13, 2021 03:40Msemaji wa jeshi al Yemen ametangaza kuwa, wapiganaji wa nchi hiyo wamefanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya kampuni ya mafuta ya Aramco na uwanja wa ndege wa Najran nchini Saudi Arabia.
-
Mahmoud Abbas: Taifa la Palestina litaendelea kuilinda Quds kwa kupambana na wavamizi
May 13, 2021 01:59Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa Quds ni mstari mwekundu na mji mkuu wa milele wa Palestina na amesisitiza uilazima wa kuendelea kutetea haki za taiifa la Palestina kwa kukabiliana na wavamizi wa Kizayuni.
-
Marekani sababu kuu ya jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapaletina
May 12, 2021 21:47Gazeti la Marekani la Washington Post limeashiria mashambulio na jinai za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) na kusema kuwa sio utawala huo tu ndio unazuia kufikiwa lengo lao tukufu la kuwa na nchi huru bali Marekani pia imekuwa na mchango mkubwa katika masaibu na matatizo ambayo yamewasibu kwa miongo kadhaa sasa.