-
Instagram yatoa tamko baada ya kufunga akaunti za waungaji mkono wa Palestina
May 09, 2021 08:08Mtandao wa kijamii wa Instagram umelazimika kutoa tamko kufuatia malalamiko ya maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutokana na kufungwa akaunti za watu walioonyesha uungaji mkono wao kwa Wapalestina wakazi wa eneo la Sheikh Jarrah Baitul Muqaddas (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.
-
Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS amwandikia barua Kiongozi Muadhamu kuhusiana na matukio ya Quds
May 09, 2021 06:21Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amemwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumjulisha matukio na mabadiliko yanayojiri katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na kutaka Ulimwengu wa Kiislamu uchukue msimamo madhubuti katika kuwaunga mkono wakazi wa mji huo mtukufu na kukomesha jinai za utawala ghasibu wa Israel.
-
Sababu za kuzuka mapigano mapya kati ya Israel na Wapalestina katika mji wa Quds
May 09, 2021 04:46Ijumaa iliyopita tarehe 7 Mei askari wa utawala haramu wa Israel walivamia msikiti mtakatifu wa al-Asqa na kuwapiga kikatili Wapalestina waliokuwa wanatekeleza ibada zao katika msikiti huo. Shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina limesema Wapalestina wasiopungua 205 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.
-
Hatimae Arab League yajitutumua kujadili jinai za utawala wa Kizayuni
May 09, 2021 01:20Hatimaye Jumuiya ya nchi za Kiarabu (Arab League) imeamua kuitisha kikao cha kuchukua maamuzi kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel kufuatia ombi la Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
-
Palestina yataka kuitisha mikutano ya kimataifa kujadili uhalifu wa Israel huko Quds
May 08, 2021 21:44Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa wito wa kuitisha mikutano ya dharura ya kimataifa ili kujadili uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
-
Imarati yatakiwa kuangalia upya uhusiano, mapatano yake na Israel
May 08, 2021 07:50Muungano wa Muqawama Dhidi ya Kuanzishwa Uhusiano na Israel wa Umoja wa Falme za Kiarabu umeitaka serikali ya Imarati, wafanyabiashara na shakhsia huru wa nchi hiyo ya Kiarabu kuangalia upya mapatano ya ushirikiano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya UAE na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Saudia yaua raia Wayemen waliokuwa wakielekea katika maandamano ya Siku ya Quds
May 08, 2021 03:36Raia wasiopungua saba wameuawa nchini Yemen katika mkoa wa Majzar baada ya ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia kushamabulia raia waliokuwa wanajitayarisha kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds jana Ijumaa.
-
Umoja wa Mataifa wasisitiza ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi ni kinyume cha sheria
May 07, 2021 23:28Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kufurusha makumi ya familia za Wapalestina katika mtaa wa Sheikh Jarrah huko Quds Mashariki na vile vile hatua ya walowezi wa Kizayuni ya kuvamia na kukalia kwa mabavu nyumba za Wapalestina na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa inazichukulia shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi na kuharibiwa nyumba za Wapalestina kuwa kinyume cha sheria za kimataifa.
-
Maandamano ya Siku ya Quds yafanyika katika baadhi ya miji ya Iraq
May 07, 2021 09:53Licha ya vizuizi vilivyowekwa kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona na kutolewa tangazo la kutofanyika maandamano na mikusanyiko kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds, wananchi wa Iraq wamefanya maandamano katika baadhi ya miji ya nchi hiyo kuadhimisha siku hiyo kwa sura ya misafara ya magari na mijumuiko ya watu.
-
Ansarullah: Kupambana na tishio la Israel, ni jukumu la kidini la Umma wa Kiislamu
May 06, 2021 23:31Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kukabiliana na vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel ni wajibu na jukumu la kidini la Umma wote wa Kiislamu.