-
Hizbullah ya Iraq: Wazayuni na Marekani wakiishambulia Saudia, tutakuwa wa mbele kuihami
May 06, 2021 21:52Msemaji wa harakati ya muqawama ya Kataeb Hizbullah ya Iraq amesema, misingi ya muqawama haiwezi kubadilika na akabainisha kuwa, endapo Saudi Arabia itakabiliwa na hatari ya kushambuliwa na Wazayuni na Marekani, mhimili wa muqawama utakuwa wa mbele kuliko yeyote yule kuihami nchi hiyo.
-
Nukta za kipekee za Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka 2021
May 06, 2021 21:49Siku ya Kimataifa ya Quds katika mwaka huu wa 2021 imewadia wakati ambao kunashuhudiwa matukio muhimu katika medani za kisiasa za muqawama au mapambano ya Kiislamu kwa upande mmoja na mikakati ya kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel katika upande wa pili.
-
Hizbullah: Ukombozi wa Quds umekaribia zaidi ya wakati wowote ule
May 06, 2021 08:15Mkuu wa Baraza Kuu la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema ukombozi wa Quds tukufu umejongea wakati huu, kuliko wakati mwingine wowote ule.
-
EU: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina ni kinyume cha sheria
May 06, 2021 03:49Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, ujenzi wa vitengoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina ni haramu na unapaswa kusitishwa.
-
Kushindwa kuunda baraza jipya la mawaziri; mwisho wa Netanyahu au kuendelea mkwamo wa kisiasa Israel
May 05, 2021 21:58Benjamin Netanhayu ameshindwa kuunda baraza jipya la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kumalizika muhula wa siku 28 alizopewa.
-
Sheikh Abdul-Fattah Mourou: Lengo la Siku ya kimataifa ya Quds ni kuwakumbusha Waislamu kuhusu kadhia yao kuu
May 05, 2021 21:56Sheikh Abdul-Fattah Mourou, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kiislamu cha al-Nahdha cha Tunisia amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds iliyotangazwa na Imam Ruhullah Khomeini (MA) mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lengo lake ni kuwakumbusha Waislamu kuhusiana na kadhia yao kuu.
-
Imran Khan aitaka OIC kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu
May 05, 2021 09:23Waziri Mkuu wa Pakistan amezitaka nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kupambana ipasavyo na wimbi la propaganda chafu dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na kusema, ni makosa na ukosefu wa uadilifu kuufungamanisha Uislamu na ugaidi.
-
HAMAS: Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya vita vya haki dhidi ya batili
May 04, 2021 22:12Mahmoud al Zahar, mjumbe mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds (Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani ambayo mwaka huu itasadifiana na Ijumaa ya keshokutwa ya tarehe 7 Mei) ni nembo ya mapambano ya haki dhidi ya batili na kusisitiza kuwa, shabaha ya kutangazwa siku hiyo ni kufanikisha ukombozi wa Palestina.
-
Makundi ya Muqawama Palestina yauonya utawala wa Kizayuni wa Israel
May 04, 2021 21:48Makundi ya muqawama na kupigania ukombozi wa Palestina yametoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuchukua hatua zozote za kuwakandamiza vijana Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
-
Madai ya Rais Biden ya kudhoofika al-Qaeda na kukabiliana na ugaidi
May 04, 2021 06:34Rais Joe Biden wa Marekani Jumapili iliyopita alidai sambamba na kuanza kuondoka askari wa Marekani nchini Afghanistan baada ya miongono miwili kwamba, Washington itaendelea kufuatilia nyendo za magaidi na kusambaratisha aina yoyote ile ya tishio la ugaidi nchini Afghanistan.